Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SERVING OTHERS, au KUWAHUDUMIA WENGINE.
Tupo hapa duniani kwa ajili ya wengine, na wengine wapo hapa duniani kwa ajili yetu. Kwa kifupi ni kwamba ili maisha hapa duniani yaende, tunayegemeana.
Hivyo, jambo pekee la kiungwana tunaloweza kufanya na maisha yetu hapa duniani, ni KUWAHUDUMIA WENGINE.
Kufanya kitu ambacho kitaboresha maisha ya wengine, na kuongeza thamani kwao ni jambo la msingi sana kwenye haya maisha yetu.
Watu wengi wamekuwa wakifikiria wafanye nini na maisha yao, na jibu la uhakika ni kuwahudumia wengine, kuwa wa msaada kwa wengine, kwa chochote unachoweza kufanya pale ulipo sasa.
Unapokuwa wa msaada kwa wengine pia unapata ridhiko la nafsi yako, kwa sababu utaona namna juhudi zako zimefanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.
Na pia, kuwahudumia wengine kutakuondolea kabisa hofu ya fedha, huwezi kukosa fedha kama kweli umejitoa kuwahudumia wengine.
Hichi kiwe kipaumbele cha maisha yetu,
Kuwahudumia wengine,
Kuwa msaada kwa wengine,
Kufanya jambo ambalo litaboresha maisha ya wengine, popote pale ulipo.
Nakutakia siku njema sana ya leo, nenda kawe wa msaada kwa wengine wengi.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info