💥 #TAFAKARI YA LEO; ONE LIFE….
Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni siku mpya ya wiki mpya ambapo tumepata fursa nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.


Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi hii tutafakari kuhusu ONE LIFE,
Maisha uliyonayo ni hayo unayoishi sasa,
Hayo ndiyo maisha unayomiliki na unayopaswa kuyatumia vizuri.
Lakini jambo moja la kushangaza ni kwamba, wapo wengi ambao hawayapi uzito maisha yao.
Wengi wanaishi maisha yao kama vile wanayajaribu kwanza, kama vile wanaonja halafu baadaye watapewa maisha kamili.
Kwa namna hii watu wanaipoteza fursa hii nzuri na ya kipekee ya maisha.

Rafiki, maisha uliyonayo ni fursa ya kipekee, ambayo haitajirudia tena kwenye dunia hii.
Hivyp itumie fursa hii vizuri, ishi kwa ukamilifu.
Kila unachotaka kufanya fanya, wala usisubiri mpaka utakapojiona upo tayari.
Hapo ulipo sasa tayari umekamilika, hakuna unachohitaji ambacho umekosa ndani yako.
Kazi yako ni moja, kutumia kila rasilimali iliyopo ndani yako, vipaji, uwezo, jitihada, ubunifu. Na pia rasilimali zilizopo nje yako ili kuweza kufanya makubwa.

Maisha uliyonayo ni hayo unayoishi, yaishi vizuri.
Nenda kaisha leo rafiki.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info