Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matoke bora.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu BE THE BEST au kuwa bora sana kwenye kile ambacho unakifanya.
Kitu chochote ambacho unafanya, chochote ambacho unaruhusu mikono yako ishike, chochote ambacho jina lako litaambatana nacho, basi kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
Hakikisha unakifanya kwa ubora wa hali ya juu,
Hakikisha wewe unakuwa bora sana kwenye kufanya kitu hicho.
Hii ndiyo njia pekee ambapo dunia itatambua uwepo wako,
Na kwa namna hii, hutakuja kulalamikia kipato.
Mara zote, kipato kinaendana na thamani ambayo mtu unatoa.
Ukiwa bora sana, unatoa thamani kubwa na hivyo kutengeneza kipato kikubwa.
Kuwa bora kunaanza na wewe kujali kile unafanya, kuwajali wale wanaokitegemea na kuona nafasi kubwa zaidi kwako kutoa thamani kwa wengine.
Vilivyo bora vinaonekana vyenyewe, vya kawaida vinamezwa kwenye kundi kubwa la vitu cya kawaida.
Kuwa bora ujitenge na kundi kubwa la walio kawaida.
Inahitaji kazi, uvumilivu na kuwa na maono makubwa.
Nenda kawe bora sana leo rafiki yangu.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info