Ukweli ni kwamba, watu wamekuwa wanaua biashara zao wao wenyewe, bila ya kujua kama wanafanya hivyo. Na hili linakuwa changamoto kwao kwa sababu wanakuja kustuka mambo yakiwa yameshaharibika sana. Wateja wameshaondoka, hasara imeshakuwa kubwa na hakuna namna ya kuiokoa tena biashara ile.
Mimi ninachotaka kukuambia leo ni uanze kuiua biashara yako wewe mwenyewe, kwa kujua kabisa unaiua, na hii inakusaidia kuiokoa biashara yako, inaifanya biashara iendelee kuwepo na iwe bora zaidi.
Wale wanaoziua biashara zao bila kujua, wamekuwa wanaendesha biashara kwa mazoea, kwa kuruhusu mambo yaende kama yanavyoenda, na kutokuifuatilia biashara kwa ukaribu. Kinachotokea huduma zinatolewa hovyo, wateja hawaridhiki, hasara zinakuwa kubwa na biashara inakufa. Wengine wanaiona fursa hiyo na kuanzisha biashara zinazotoa huduma bora zaidi na hivyo kumalizia kabisa kifo cha biashara.
Kwa kuiua biashara yako mwenyewe, maana yake unaiangalia biashara yako kwa karibu, unaangalia wapi ambapo panahitaji marekebisho na unafanya hivyo mapema, kabla hata mteja hajajua. Unachofanya ni kuibadili na kuiboresha biashara kabla hata mteja hajaona kile anakosa na kuanza kutafuta kwa wengine.
SOMA; Anza Kuwa Bora Wewe Kwanza…
Unaweza kuona dhana hii siyo kuua biashara, bali ndiyo kitu unapaswa kufanya kwenye biashara yako kila siku. Na ni kweli kabisa, lakini unajua nini, wengi hawafanyi hivyo. Na mtu yeyote anayetaka kufanya biashara kama yako, anachoanza kuangalia ni mapungufu yako, na yeye anayafanyia kazi. Mwishowe wateja wanatoka kwako na kwenda kwa yule anayekuwa bora, kinachotokea ni biashara yako kufa.
Hivyo basi, njia ya wewe kupona kwenye biashara, ni kuwa wa kwanza kuiua biashara yako, yaani kuiangalia biashara yako kama ambavyo mshindani wako anaiangalia. Kuangalia wapi una mapungufu na kuyafanyia kazi. Kuangalia wapi watu hawaridhishwi na kuwapa kile ambacho kinawaridhisha.
Kwa kuwa wa kwanza kuua biashara yako, unaisaidia, unaiboresha na mwisho kabisa unajikuta ukiwa na biashara bora kabisa, ambayo ni tofauti kabisa na ile uliyoanza nayo. Na wanaojaribu kukuua, wanakosa pa kugusa, maana wewe mwenyewe upo bize kuiua biashara yako.
Chukua hatua kabla watu hawajaichukulia hatua biashara yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Lakini cocha du u think unaweza ukaona weaknes zako??? For how ?
LikeLike
Ukiwa makini na biashara yako,
Ukiwa mtu wa kujihoji na kudadisi zaidi,
Ukiwa mtu wa kujifunza kila siku,
Na ukiwa mtu wa kusikiliza wengine wanasemaje, hasa malalamiko ya wateja, utaona weakness zako nyingi mno na utaweza kuzifanyia kazi.
Ila kama hutakuwa na hayo hapo juu, utakuwa umejifungia kwenye ulimwengu wako mwenyewe na kujiangamiza mwenyewe.
LikeLike