Unapokuwa mfanyabiashara, maisha yako unayajenga kwenye msingi wa kuuza vitu, yaani unapata kipato cha kuendesha maisha, kupitia kile unachouza.
Sasa kwa kuwa hayo ni maisha, lazima uwe makini sana kwa sababu kosa dogo unaloweza kufanya, litakuwa na madhara makubwa sana kwako. Wapo watu ambao wameharibu biashara zao kwa makosa madogo ambayo hawakuyafikiri kwa kina. Hasa pale wanapojaribu vitu vipya ambavyo hawajawahi kuuza.
Sheria ya kwanza kabisa ya chochote unachotaka kuuza ni je kinafanya kazi? Je kinawasaidia watu kutatua matatizo yao? Je kinatimiza mahitaji yao. Na muhimu zaidi je kwa kukinunua leo watarudi tena wakati mwingine wanapokuwa na uhitaji?
Usikimbilie tu kuuza kitu kwa sababu watu wanasema ni fursa au kwa kuwa ni kitu kipya kimeingia, jiulize je kinafanya kazi? Anzia hapo kama unataka kudumu kwenye biashara unayofanya.
SOMA; Maisha Yako Ni Kazi Inayoendelea….
Japokuwa hii inaweza isifae kwa biashara zote, lakini kipimo kizuri je wewe ungekuwa tayari kununua? Kwa gharama iliyowekwa, na kwa matumizi ya kitu hicho, je wewe ungekuwa tayari kununua kwa mwingine anayeuza? Kwa kujiweka kwenye viatu vya mteja, itakuwa rahisi kwako kuona kama upo kwenye njia sahihi au la.
Kama hakifanyi kazi, kama mteja hatakuwa tayari kurudi tena kwako, au kuwaambia wengine kuhusu wewe, usikiuze, hata kama kila mtu anauza.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog
