Hizi Ndiyo Mada Zitakazofundishwa Kwenye Semina Ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, Usipange Kuikosa.

Habari za leo rafiki,

Tangu mwezi uliopita, nimekuwa nakupa taarifa za semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION) ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap kwenye KISIMA CHA MAARIFA.Kwenye semina hii, nilifanya tofauti kidogo, nilikuomba wewe rafiki yangu, uniambie ni kitu gani ungependa kujifunza kuhusu fedha. Na nikushukuru sana kwa ushirikiano wako, maana nilipokea maoni mengi mno, mengi sana na mazuri.

Baada ya kuyapitia maoni yote kwa kina, na kuangalia dira ya semina hii niliyoandaa, nimekamilisha mada nitakazofundisha kwenye semina hii. Na hivyo nachukua nafasi hii kukupa mada hizi ili uweze kujiandaa kupokea elimu hii ya kujijengea msingi wa fedha.

MUHIMU; Nimejitahidi kuhakikisha angalau yale ya msingi kabisa kuhusu fedha yanakuwepo. Kama kuna ambayo ungependa kujifunza na hayapo kwenye mada hizi, usiwe na wasiwasi, utauliza kama maswali wakati wa semina na nitakupa majibu. Hivyo pitia mada hizi na karibu sana kwenye semina.

SEMINA; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION)

FEDHA; DHANA HALISI YA FEDHA, UTAJIRI NA UHURU WA KIFEDHA.


Maana halisi ya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha.

Mahusiano ya fedha na imani.

Jinsi unavyojizuia kupata fedha zaidi.

Kwa nini elimu ya darasani ni kikwazo kwenye fedha.

Namna ya kutengeneza fursa zaidi za kifedha kwenye maisha yako.

Sheria tano za fedha unazopaswa kuzijua na kuzisimamia.

KIPATO; NJIA ZA KUTENGENEZA KIPATO NA KUKIONGEZA.


Msingi muhimu wa kutengeneza kipato.

Umuhimu wa mifereji mingi ya kipato.

Mifereji ya kipato unayopaswa kuitumia.

Jinsi ya kukigawa kipato chako kwenye mafungu matano muhimu kwako.

Jinsi ya kudhibiti kipato kikubwa kinachoingia kwa mara moja.

Jinsi ya kuongeza kipato ukiwa hapo ulipo sasa.

MATUMIZI; JINSI UNAVYOWEZA KUDHIBITI MATUMIZI YAKO NA KUWA NA MAISHA BORA.

Jinsi ya kutambua matumizi muhimu na yasiyo muhimu.

Panga matumizi kabla hujapokea fedha unayotegemea.

Jinsi ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora.

Gharama zilizojificha ambazo zinaongeza matumizi yako.

Jinsi ya kuzuia matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka.

Jinsi ya kuepuka kurudishwa nyuma na utegemezi mkubwa.

MADENI; NAMNA YA KUONDOKA KWENYE MADENI NA KUEPUKA KUINGIA KWENYE MADENI MABAYA.


Madeni ni utumwa.

Madeni mazuri na madeni mabaya.

Jinsi ya kuondoka kwenye madeni.

Jinsi ya kuepuka kuingia kwenye madeni.

Kigezo muhimu cha kuzingatia pale unapofikiria kukopa.

BIASHARA; NJIA YA UHAKIKA YA KUTENGENEZA KIPATO KISICHO NA UKOMO.


Msingi muhimu wa biashara unaopaswa kuuelewa.

Kwa nini kila mtu anapaswa kuwa na biashara.

Kuanza biashara ukiwa chini kabisa.

Biashara unayoweza kuanza kufanya.

Mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara yako.


UWEKEZAJI; NJIA YA KUIFANYA FEDHA IKUFANYIE WEWE KAZI, INGIZA KIPATO HATA KAMA UMELALA.

Maana ya uwekezaji na umuhimu wake kwenye uhuru wa kifedha.

Dhana ya COMPOUND INTEREST na RULE OF 72 na namna ya kuzitumia kufanikiwa kwenye uwekezaji.

Tofauti ya uwekezaji mzuri (ASSETS) na uwekezaji mbaya (LIABILITIES)

Aina tano kuu za uwekezaji unazopaswa kuzijua.

Jinsi ya kupangilia uwekezaji wako ili kuwa na uhuru wa kifedha.

Uwekezaji unaopaswa kuanza nao mara moja.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji ili kufanikiwa kifedha.


KODI; MISINGI YA KODI NA NJIA ZA KUPUNGUZA KODI.


Maana halisi ya kodi na umuhimu wake kwa maendeleo.

Kodi zinazokuhusu wewe moja kwa moja.

Jinsi unavyoweza kupata unafuu wa kodi.


BIMA; NJIA ZA KULINDA FEDHA NA MALI ZAKO.


Maana ya bima na umuhimu wake kwenye uhuru wa kifedha.

Bima unazopaswa kuwa nazo kwenye maisha yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia unapochagua bima.


WATOTO; JINSI YA KUWAJENGEA WATOTO MSINGI MZURI WA KIFEDHA.


Umuhimu wa kuwajengea watoto msingi wa kifedha.

Umri sahihi wa kuanza kuwajengea watoto misingi ya kifedha.

Misingi ya kifedha ambayo unapaswa kuwajengea watoto wako.

Jinsi ya kuwafuatilia watoto kwenye elimu na misingi ya kifedha.

Kuwashirikisha watoto kwenye shughuli zako za kifedha.


KUTOA; MAISHA YA UTAJIRI YENYE MANUFAA KWA WENGINE.


Utajiri siyo kwa ajili yako mwenyewe, ni kwa ajili ya jamii.

Kuacha wosia na mgawanyo mzuri wa mali zako baada ya kifo chako.

Njia bora za kutoa utajiri wako kwa wengine.

Utoaji wa sadaka na mafungu mengine muhimu kulingana na imani yako.

Hizo ndizo mada za semina hii nzuri rafiki, nina imani tutakuwa pamoja kwenye semina hii. Na kama kuna ambalo ungependa kujifunza ila hujaliona hapo, usiwe na shaka, utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali na utajibiwa.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kufaidi semina hii, basi maelekezo yako hapo chini;

KARIBU UJIFUNZE ELIMU YA MSINGI YA FEDHA MWEZI WA SABA.

Mwezi wa saba mwaka 2017, nimeandaa semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION). Hii ni semina ambayo nitaiendesha kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo Tanzania na hata duniani. Huhitaji kusafiri au kuacha kazi zako, unachohitaji ni kutenga muda wako mfupi kila siku wa kufuatilia semina hii.

Ili kuweza kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa mwanachama unaweza kusoma makala nyingi kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni ya wanachama tu, pia unakuwa kwenye kundi la wasap ambapo kila siku unapata tafakari na kila jumapili tunakuwa na madarasa ambapo tunajifunza mambo muhimu kuhusu mafanikio.

Kuwa mwanachama unapaswa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= ambapo ada hii inakwenda kwa mwaka mmoja tangu siku unayolipa. Ada inalipwa kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina Amani Makirita. Ukishalipa ada tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 na nitakuweka kwenye kundi.

Semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, siyo semina ya kukosa kwa mtu yeyote yule ambaye yupo makini na maisha yake. Fanya malipo leo ili uweze kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii ya kipekee sana kwako.

Karibu sana tujenge msingi imara wa kifedha kwetu na kwa vizazi vyetu. Chukua hatua kwa kufanya malipo leo ili kuweza kushiriki semina hii nzuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu


Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: