Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera kwa siku hii bora sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu PESA HAILALI,
Rafiki yangu,
Pesa haijui usiku wala mchana,
Pesa haijui muda,
Peaa haijui majira,
Pesa haijui sikukuu,
Pesa haijui mwisho wa wiki,
Na wala pesa haijui kuhusu ratiba zozote zile.
Pesa inajua kitu kimoja tu….THAMANI.
Pia pesa inapenda kuzungushwa,
Na muhimu zaidi, pesa inapenda kutumwa.
Hivyo rafiki, katika mipango yako yote ya fedha, lazima uzielewe sofa hizi za fedha, ili…
Uweze kuwa na mfumo ambao unatengeneza fedha bila ya kujali muda.
Uweze kuizungusha fedha kila wakati.
Uweze kuitumikisha fedha ili ikupe kile unachotaka.
Kwa kukosa mfumo wa aina hiyo, utaishia kuwashikia wengine fedha, kwa kuzipata lakini zikakuponyoka zote.
Pia pesa itakutumikisha sana kama wewe utashindwa kuitumikisha.
Yote haya yanaanza na wewe mwenyewe rafiki.
Uwe na siki njema sana.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.