Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Umeianzaje siku hii nyingine nzuri ya leo?
Umejipangaje kuhakikisha kwamba siku hii inakuwa bora zaidi kwako?
Je msingi muhimu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA unaufanyia kazi kila siku?

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu GAMING THE SYSTEM…
Kila jambo tunalofanya kwenye maisha yetu, lipo katika mfumo fulani.
Iwe ni kazi, biashara, maisha, mahusiano na kadhalika…
Kila mfumo una namna ambayo mtu anaweza kupita njia ya mkato na kupata kile anachokitaka.
Lakini changamoto kubwa ni kwamba njia hizo huwa hazidumu.
Ni njia ambazo zinaleta matokeo kidogo na yanayodumu kwa muda mfupi.
Njia pekee inayoleta matokeo bora na yanayodumu milele, ni njia sahihi, isiyokuwa ya ujanja ujanja wala mkato.

Hivyo rafiki, kila unaposhawishika kuchukua njia ya mkato,
Kila unapoona njia ya mkato itakusaidia haraka,
Jikumbushe hili na achana na njia hiyo.
Unaweza kupata hicho unachofikiria kupata kwa muda mfupi, ila ukaharibu kila kitu kwa muda mrefu.

Usijaribu kuutega na kuuchezea mfumo wowote kwenye maisha yako. Hautakuacha salama.
DO NOT GAME THE SYSTEM, PLAY THE LONG GAME. Ushindi halisi ni ule unaopatikana kwa kufanya vitu sahihi kwa njia sahihi. Fanya hivyo.

Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info