Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo rafiki yangu.
Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NJIA YA KUTAJIRIKA HARAKA BILA KAZI…
Hichi ni kitu ambacho watu wamekuwa wanaumizwa nacho kila kizazi…
Kwenye kila kizazi, huwa wanaibuka watu ambao wanawashawishi wengine kwamba kuna njia ya kutajirika haraka bila ya kufanya kazi.
Watu wamekuwa wabakubali hilo na kuishia kutapeliwa au kupotezewa muda wao.
Mambo unayopaswa kujua bila ya kusita au kuwa na shaka no haya;
1. Haipo na wala haitakuja kuwepo njia ya kutajirika haraka bila ya kufanya kazi. Haipo kabisa, wala usimsikilize anayekuambia ipo.
- Kama njia hiyo ingekuwepo, watu wangekuwa bize kuitumia wala wasingekukumbuka wewe. Binadamu ni wabinafsi, kikitokea kitu kizuri, watajinufaisha kwanza wao wenyewe kabla hawajakuletea na wewe.
-
Chochote ambacho unaweza kufanya na kikakuletea fedha za haraka, bila ya kuweka juhudi, fedha hizo zitaondoka bila ya kufanya la maana kwako.
Sasa wengi wanayajua hayo nimesema hapo juu, lakini huwa wanaruhusu hisia zitawale fikra,
Hivyo anapokuja mtu na hadithi zake za utajiri wa haraka bila kazi, wanasema siyo kweli. Lakini watu hao, huwa wamejipanga vizuri, kwa sababu wanajua utawakatalia, hivyo wanakuja na mifano, ona huyu alianzia chini kabisa sasa hivi yupo juu. Na hapo ndipo unanasa kama samaki, unaanza kushawishika labda wewe ndiye unayekosea. Unaona labda ujaribu tu mara moja na uone kama ni kweli. Na hapo unakuwa umeingia kwenye mtego na kutapeliwa.
Jua msingi huwa haibadiliki, hata kama dunia nzima inabadilika. Hivyo kaa mbali kabisa na anayepindisha miaingi. Ukiendelea kumsikiliza, atakuhadaa ukajikuta unataka kujaribu kitu na kuishia kutapeliwa.
Usikubali kabisa kuhadaiwa na vitu ambavyo kimsingi havifanyi kazi.
Uwe na siku bora sana ya leo rafiki.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info