Hongera rafiki kwa siku hii ya kipekee na nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu DAY ONE yaani SIKU YA KWANZA…
Rafiki, hebu leo jikumbushe siku ya kwanza kwako kufanya jambo lolote kwenye maisha yako…
Kumbuka siku ya kwanza unakwenda kuanza shule, ni hamasa kiasi gani uliyokuwa nayo, huenda hata hukulala vizuri, ukisubiri kwenda shuleni.
Kumbuka siku ya kwanza unakwenda kuanza kazi yako, ulikuwa na hamasa kubwa sana ya kuweka juhudi kubwa kwenye kazi hiyo.
Kumbuka siku ya kwanza unaanza biashara yako, ulimwona mteja kama mtu muhimu mno kwako.
Kumbuka siku ya kwanza unakutana na mwenza wako, muda wote ulikuwa unafikiria kuhusu yeye tu.
Kumbuka siku ya kwanza kusafiri kwenda sehemu tofauti na uliyozoea, safari nzima ilikuwa burudani kwako…
Lakini siku zinazofuatia baada ya hapo,
Tunazoea mambo,
Tunachukulia kawaida,
Hamasa ya mwanzo inapungua,
Tunaona ni kitu ambacho kipo tu,
Na hapo ndipo ufanisi wetu unaposhuka,
Na kupoteza nafasi yetu ya kufanikiwa.
Tukichukua mfano wa biashara,
Wafanyabiashara wengi huwa na hamasa kubwa siku ya kwanza,
Huweka juhudi kubwa sana,
Hufanya kazi kwa muda mrefu,
Huwashawishi wateja wanunue, na kuwapa huduma bora sana.
Wateja wanafurahia na kupenda biashara ile.
Biashara inaanza kuonesha mafanikio,
Mwenye biashara anaanza kuridhika,
Anaanza kupungiza ile kasi aliyokuwa nayo mwanzo,
Anaona ameshapata kile alitaka,
Wateja wanaanza kupata huduma mbovu,
Hawaridhishwi,
Na wanaanza kutafuta mahali pengine pa kupata huduma wanazotaka.
Biashara inaingia kwenye changamoto…
Rafiki,
Kitu chochote unachofanya kwenye maisha yako, kila siku kifanye kama ndiyo SIKU YA KWANZA KUKIFANYA.
Tumia viwango vya DAY ONE kwenye maisha, kazi, biashara, mahusiano na kila kitu unachogusa.
Usiruhusu ile hamasa ya mwanzo ipotee kwa namna yoyote ile.
Usikubali kuzoea kitu chochote kile.
Ishi kila siku yako kama siku ya kwanza,
siku ambayo ni ya hamasa, ambayo unaweka juhudi kubwa sana.
Leo bi siku ya kwanza rafiki, unaitumiaje?
Kumbuka, siku ya pili ni siku ya kupotea, usiishi siku ya pili, ishi siku ya kwanza kila siku.
Uwe na siku njema sana ya leo.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info
ONE….