Habari rafiki?
Napenda kuchukua nafasi hii kukupa taarifa za semina ya KISIMA CHA MAARIFA itakayofanyika mwezi oktoba mwaka 2017. Semina hii itakuwa ya kuhudhuria moja kwa moja na itafanyika jijini dar es salaam.



Hii ni semina ya wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, ambapo kwa pamoja tutakutana, kujifunza na kukuza mahusiano baina yetu ili kukuza mitandao yetu ya kibiashara na mafanikio. Hivyo ni muhimu kwa kila mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA kuhudhuria semina hii.

Semina itafanyika jumamosi ya tarehe 28/10/2017, jijini dar es salaam, eneo kamili nitawafahamisha baadaye.

Semina hii itakuwa ya masaa 12 kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa 2 usiku. Tutakuwa na masaa 10 ya kujifunza na kushirikiana na masaa mawili ya kula na kupumzika.

Ni semina ambayo itakuwa na mambo mengi ya kujifunza pamoja na kushirikiana katika vikundi vidogo vidogo.

Mada za semina.

Kwa kuwa lengo kuu la KISIMA CHA MAARIFA ni kila mmoja wetu kupiga hatua na kufanikiwa, na pia kwa kuwa moja ya vigezo vya kuendelea kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni kuwa na biashara pamoja na uwekezaji, semina hii itatuwezesha kujenga misingi imara kwenye maeneo hayo muhimu.

Mada kuu zitakazofundishwa kwenye semina hii zitakuwa tatu;

Moja; kuongeza kipato na kuongeza mifereji ya kipato.

Mbili; usimamizi bora wa biashara na kuongeza mauzo.

Tatu; usimamizi bora wa kilimo na kuongeza thamani.
Pia tutakuwa na kipindi cha kukaa ndani ya vikundi vidogo vidogo, kushirikiana kwenye mambo mbalimbali na hata kuendelea kufuatiliana baada ya semina.

Tutapata shuhuda na uzoefu kutoka kwa baadhi ya wanachama wenzetu wa KISIMA CHA MAARIFA, kupitia yale wanayofanya, walikoanzia, walipo sasa na wanapoelekea.

Walimu wa semina.

Semina hii itakuwa na mafunzo mbalimbali kama nilivyoeleza hapo juu. Hivyo pia tutahitaji kuwa na wataalamu na wazoefu kwenye baadhi ya mambo tunayokwenda kujifunza kwenye semina hii.

Katika semina hii nitakuwa na walimu wengine wawili ambao watafundisha, walimu hawa ni wazoefu kwenye yale wanayokwenda kutufundisha na kutushirikisha.

Kitakachoendelea baada ya semina.

Semina hizi za kukutana kwa pamoja za KISIMA CHA MAARIFA, itakuwa inafanyika moja kila mwaka. Hivyo baada ya semina hii ya oktoba 2017, itakayofuata itakuwa ya oktoba 2018. Lakini hapo katikati tutakuwa na semina nyingine ndogo ndogo za ufuatiliaji wa utekelezaji wa yale ambayo tumejifunza kwenye semina na kupanga kuchukua hatua.

Kwenye semina hii, tutatengeneza vikundi vya watu kulingana na ukaribu wao kwa wanakoishi, inaweza kuwa kimkoa au kwa mikoa ya karibu. Kila kikundi watawekeana utaratibu wa kufuatiliana na kushirikiana zaidi.

Pia kwenye kila kikundi wataandaa semina moja kati ya miezi mitano mpaka nane baada ya semina hii, ambapo mimi nitahudhuria semina hiyo ndogo kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kila mwanachama pamoja na kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo.

Semina hizi zitaandaliwa kwa yale maeneo waliyopo wanachama na mimi nitasafiri kwenda kwenye semina hizo.

Ada ya kushiriki semina.

Semina hii itakuwa ndefu, ya siku nzima kwa sababu ni tukio moja kubwa la mwaka la sisi kukutana pamoja na kujifunza.

Kutakuwa na huduma mbalimbali, kuanzia chai, chakula pamoja na vitafunwa vya jioni.

Kutakuwa pia na maandalizi ya vitu mbalimbali ambavyo tutatumia kwenye semina, kama vitabu maalumu kwa ajili ya semina vya kuandika mafunzo na kuweka mipango.

Ili kuweza kukamilisha gharama zote hizo, kila mwanachama atachangia tsh 50,000/= kama ada ya kushiriki semina hii.

Ada ya semina itaanza kulipwa kuanzia tarehe 01/10/2017.

Jiandae na semina.

Rafiki, nimetoa taarifa hizi mapema sana, miezi zaidi ya miwili kabla ya siku ya semina ili kila mmoja wetu apate nafasi ya kujiandaa na kuweza kushiriki semina hii.

Kwa wale watakaosafiri waweze kujiandaa vizuri, kwa wanaohitaji kuomba ruhusa pia waweze kufanya hivyo mapema.

Kwa wale wenye kuandaa mazingira mazuri ya shughuli zao ili ziweze kwenda vizuri wakati wamesafiri kwa ajili ya semina nao waweze kufanya hivyo pia.

Sitegemei hata mtu mmoja kukosa semina hii, kwa sababu ni hitaji la kila mmoja wetu kupiga hatua, na semina hii ni sehemu muhimu ya kuwezesha hilo.

Dhibitisha kushiriki semina.

Kama wewe tayari ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, kwa maana kwamba umeshalipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, kwenye kundi la Telegram la 

KISIMA CHA MAARIFA nimetoa maelekezo ya kudhibitisha kushiriki.

Kama bado hujawa mwanachama, basi unahitaji kujiunga kwanza na KISIMA CHA MAARIFA ndiyo upate nafasi ya kushiriki semina hii ya oktoba. Kwa sababu hii ni semina maalumu kwa wanachama, ili tuweze kufuatiliana vizuri. Sitaki uhudhurie semina, ufurahie tu mafundisho halafu ukaendelee na maisha yako. Nataka tufuatiliane kwa mwaka mzima, ndiyo maana itakupasa ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Kujiunga tuwasiliane kwa ujumbe wa njia ya wasap 0717 396 253 ujumbe uwe na neno 

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017.

Karibuni sana wote tujifunze kwa pamoja kwa tukio hili kubwa linalotokea kwa mwaka mara moja.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.