#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO.
KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems.
Kurasa 21 – 31.
Nini maana ya maisha mazuri?
Swali moja ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kuhusu maana ya maisha mazuri.
Kumekuwepo mijadala mingi kuhusu nini maana ya maisha mazuri na mambo gani yanachangia maisha mazuri.
Maisha mazuri ni pale mtu anapokuwa na maana ya maisha yake.
Na hili ni changamoto kwa sababu maana ya maisha inakuwa tofauti kwa watu tofauti.
Hivyo hakuna njia moja au maana moja ya maisha kwa watu wote.
Na hii ndiyo sababu serikali au taasisi zote ambazo zimekuwa zinawataka watu kuamini kitu kimoja, iwe ni itikadi, dini, sayansi au falsafa hukutana na changamoto kubwa.
Katika falsafa na utamaduni wa Socrates zipo hatua kuu nne za kufikia maisha mazuri.
1. Sisi kama watu tunaweza kujijua wenyewe. Tunaweza kutumia uwezo wetu wa kufikiri kujua imani zetu na maadili yetu.
2. Sisi watu tunaweza kubadilika wenyewe. Tunaweza kutumia fikra zetu kubadili mawazo yetu na imani zetu, na hili litabadili hisia zetu.
3. Sisi watu tunaweza kutengeneza tabia mpya kwa namna tunavyotaka wenyewe.
4. Kama tukifuata falsafa kama njia yetu ya maisha, basi tutakuwa na maisha mazuri na yenye maana kwetu.
Tutumie uwezo huu mkubwa uliopo ndani yetu katika kutengeneza maisha yenye maana kwetu.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa
