#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO.
KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems.
Kurasa 33 – 45.
HALI YETU YA UDHIBITI JUU YA MAMBO YANAYOTUTOKEA.
Mambo yote yanayotokea kwenye maisha yetu tunaweza kuyagawa katika makundi mawili.
1. Mambo ambayo yapo chini ya udhibiti wetu, haya ni yale ambayo tunaweza kuyaathiri moja kwa moja, kama imani zetu na mawazo yetu.
2. Mambo ambayo hayapo chini ya udhibiti wetu, haya ni mambo ambayo hatuwezi kuyaathiri au kuyabadili, mfano watu wengine, hali ya hewa, hali ya uchumi na kadhalika.
Sasa changamoto kubwa kwenye maisha yetu zinaanza palr tunapojaribu kudhibiti mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako, na kushindwa kudhibiti yale ambayo yapo ndani ya uwezo wetu.
Hili ndiyo linaleta kila aina ya changamoto na hata magonjwa ya akili.
Kila jambo linapotokea kwenye maisha yako, au jambo lolote linaloendepea kwenye maisha yako, jiulize je lipo chini ya udhibiti wako? Kuna kitu unaweza kufanya kubadili?
Kama jibu ni ndiyo chukua hatua mara moja.
Kama jibu ni hapana basi achana nalo, kung’ang’ana na yaliyo nje ya udhibiti wako ni kujitafutia shida.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa