#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO.
KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans

UKurasa 56 – 73.

Jinsi ya kuidhibiti hasira.

Hasira ni moja ya hisia ambazo zina matokeo mabaya saba kwa yeyote anayekuwa nayo.
Upo usemi kwamba HASIRA NI HASARA, na ni sahihi kabisa kwamba hatua ambazo watu wanachukua wanapokuwa na hasira, huwa zina madhara mabaa.
Lakini wakati mwingine watu huona kama hawawezi kuzuia hasira zao.
Wengi huamini hasira zinasababishwa na wengine na hivyo hawana jinsi ya kuzitatua.
Wanafalsafa ya Ustoa wanakataa hili.
Mwanafalsafa Seneca anatuambia kwamba hasira tunazitengeneza sisi wenyewe kutokana na matarajio makubwa tunayokuwa nayo kwa wengine na dunia kwa ujumla.
Tunataka dunia iende kama tunavyotaka sisi, na watu wawe kama tunavyotaka sasa.
Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.
Hivyo kudhibiti hasira, kwanza tuiruhusu dunia iende kama inavyoenda, na watu wafanye kama wanavyofanya.

Mwanafalsafa Seneca pia anatushirikisha hatua tatu za kudhibiti hasira;
1. Jua ni vitu gani vinachochea hasira kwako, kisha panga kukaa navyo mbali au kuvichukulia kama vilivyo ili usikasirishwe.
2. Kuwa na subira, pale unapopatwa na hasira, usikimbilie kusema au kufanya chochote, badala yake kuwa na subira. Kwa njia hii akili yako inatulia na unajiepusha na matatizo zaidi.
3. Tabasamu badala ya kununa. Tunapopatwa na hasira, miili yetu hubadilika, sura hujikunja na tunanuna. Ukiweza kwenda kinyume na mwili wako, kwa kutabasamu, utailegeza hasira na kuona kile unachokasirikia hakina maana.

Wastoa wanatuambia kwamba, iwapo tutaiangalia dunia kama ilivyo, na siyo kama tunavyotaka sisi, na iwapo tutawaruhusu watu waishi kama wanavyoishi, na siyo kama tunavyotaka sisi waishi au watuchukulieje, basi hatuwezi kusumbuliwa na hasira kamwe.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa