#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO.
KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 74 – 83.

Falsafa ya ustoa na matumizi yake katika jamii.

Falsafa ya ustoa imekuwa ikichukuliwa kwa mtazamo hasi, kwamba wastoa ni watu ambao wanaficha na kukandamiza hisia zao.
Lakini ukweli ni kwamba wastoa hawakandamizi hisia, bali wanazibadilisha kwa kutumia fikra zao.
Hawakubali hisia ziwaendeshe, ila wao ndiyo wanaziendesha hisia.

Licha ya falsafa hii kupotea kwa muda mrefu, sasa imeanza kurudi na wapo wengi wanaoitumia kwenye maisha yao ya kila siku.
Wanajeshi, wanamichezo na shughuli nyingine zote ambazo ni hatari na zinahitaji ujasiri wa hali ya juu, wale ambao wamekuwa wanajifunza falsafa ya ustoa wameweza kufanikiwa.
Pia matibabu ya watu wenye matatizo ya afya ya akili, kwa kutumia njia ya CBT ambayo inahusisha fikra na tabia, imetokana na falsafa ya ustoa.

Falsafa ya ustoa imekuwa msaada kwa wengi kuelewa maana ya maisha yao na kwa nini wateseke.
Falsafa hii pia imekuwa inawaandaa watu kabla hawajakutana na mateso kamili, hivyo mateso yanakuwa siyo kitu cha kushangaza kwao.
Kama bado hujawa na falsafa ya maisha yako, nakushauri sana ufikirie kuhusu Falsafa ya ustoa. (Stoicism).

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa