KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 84 – 93..
Epicurus ni mwanafalsafa aliyeamini kwenye furaha kwenye kuishi kwenye wakati ujao.
Epicurus aliamini kwamba lengo letu hapa duniani ni kuwa na maisha ya furaha na kuepuka maumivu.
Alianzisha falsafa hii ya kuishi kwenye wakati uliopo na kufanya yale ambayo yanamletea mtu furaha. Kwa sababu maisha ya hapa duniani ni mafupi.
Falsafa ya Epicurus ilieleweka vibaya na wengine, na wengi waliipinga kwa kuamini kwamba ilihamasisha watu kuingia kwenye ulevi wa starehe. Kunywa pombe, kula vyakula na kufanya mapenzi.
Hata baadhi ya wafuasi wa Epicurus, waliamini hiyo ndiyo maana ya falsafa hiyo ambaye baadaye ilijulikana kama Epicurean. Kwamba hakuna kufanya chochote bali statehe pekee.
Epicurus alijenga falsafa yake kwenye msingi kwamba, kile unachofanya sasa, ndiyo kinakuletea furaha au maumivu. Mawazo unayokuwa nayo sasa, ndiyo yanaleta furaha au maumivu.
Watu wengi wanaangalia mambo yaloyopita, yanawaumiza na kuwaondolea furaha. Wakati huo pia wana hofu ya mambo yajayo, kitu ambacho kinawaondolea furaha pia.
Lakini hakuna unachoweza kubadili kwa kufikiria wakati uliopita au wakati ujao.
Hivyo ni vyema kuishi sasa, kufanya kile ambacho mtu unaweza kufanya sasa na kuepuka maumivu.
Epicurus aliwaasa watu kutokutegemea starehe za ulevi au mapenzi, akisema kwamba starehe za aina hiyo hupelekea watu kuwa watumwa wa vitu hivyo baadaye na kutengeneza maumivu makali.
Popote ambapo mtu upo sasa, kipo ambacho unaweza kufanya, licha ya kujali umetokea wapi, au kesho itatokea nini. Hebu tuchukue hatua hizi tunazoweza kuchukua sasa, na kuhakikisha tunakuwa na maisha yenye furaha na kuepuka maumivu.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa