Watu wengi wanaposikia soko la hisa, basi hufikiri kinachouzwa na kununuliwa ni hisa pekee. Lakini huu siyo ukweli. Kwenye soko la hisa kuna bidhaa mbalimbali za kifedha ambazo zinapatikana.
Bidhaa hizi za kifedha kwa pamoja zinajulikana kama amana. Na hizi ndizo hupatikana kwenye masoko ya hisa na njia nyingine za uwekezaji.

Kwenye soko la hisa la Dar es salaam, kuna aina mbili za amana zinazopatikana.
Aina ya kwanza ni hisa za makampuni yaliyosajiliwa kwenye soko la hisa. Hapa unawekeza kwa kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Unaichangia kampuni mtaji na hivyo unapata faida kwa njia ya gawio pale kampuni inapopata faida na/au kuongezeka kwa thamani ya hisa ulizonunua.
Aina ya pili ya amana zinazopatikana kwenye soko la hisa la Dar ni hatifungani. Hii ni aina ya uwekezaji ambapo unaikopesha kampuni au taasisi fedha, inakwenda kuzitumia kwenye shughuli zake na inakuahidi kukurejeshea fedha yako baada ya muda fulani pamoja na riba.
SOMA; Ujue Uwekezaji Kwenye Hatifungani (BONDS) Na Faida Zake.
Kwenye uwekezaji wa hatifungani, fedha yako unaiweka kwa muda fulani, ambao huwa ni muda mrefu kiasi na baada ya muda huo unapata mtaji uliowekeza pamoja na riba ambayo ilipangwa wakati unawekeza kwenye hatifungani hizo.
Kwenye makala zijazo za uwekezaji leo tutachambua zaidi kuhusu hatifungani na aina ya hatifungani zinazopatikana kwenye soko la hisa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog