KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 104 – 113.
Karibu kila jamii na kila tamaduni hapa duniani, imekuwa ikijaribu kueleza maana ya maisha na nini kinachoongoza maisha yetu hapa duniani.
Dini mbalimbali zimekuwa na kubwa ya maana ya maisha na kinachoongoza maisha hapa duniani.
Mwanafalsafa Heraclitus alikuwa mmoja wa watu walioamini na kupendekeza kwamba, dunia yote ni kitu kimoja, na sisi binadamu pamoja na vitu vyote vilivyopo hapa duniani tumeungana kwa namna fulani.
Baadaye wanasayansi walioweza kwenda angalia waliweza kudhibitisha hili, baada ya kupata fikra za tofauti walipokuwa angali.
Pia sayansi inaanza kuonesha kwamba dunia inaweza kuwa imetengenezwa na kitu kimoja, ambacho ni nguvu (energy).
Zamani iliaminika dunia imetengenezwa na udongo na maji, baadaye ikaja hewa na sasa ni nguvu.
Ukiangalia kwa undani, kila kitu hapa duniani kinaendeshwa kwa mfumo huu wa nguvu.
Mwanafalsafa Heraclitus pia aliamimi japokuwa kuna upacha wa kila kitu hapa duniani, usiku na mchana, utoto na uzee, giza na mwanga, bado kila kitu ni kizuri.
Kusema kitu fulani ni kizuri zaidi ya kingine ni kufikiri kwakutumia akili ya ushindani na kutokuielewa vizuri dunia.
Kila kitu ni kizuri kama tutakielewa na kuweza kukitumia vizuri.
Tuna kila sababu ya kushirikiana pamoja na kutunza vizuri kila kitu hapa duniani, kwa sababu kina mchango kwenye maisha yetu.
Na lolote tunalokutana nalo au kupitia, tukumbuke ni jambo zuri kama tutaweza kulitumia vyema.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa