KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 114 – 123.

Kumekuwepo na mjadala mkali baina ya wanasayansi kwa upande mmoja na wanafalsafa kwa upande wa pili.
Wapo wanasayansi wanaoamini kwamba falsafa imekufa na kwamba chochote ambacho falsafa inasimamia hakina msingi.
Wanasayansi hawa wanashindwa kujibu swali la kwa nini binadamu tuna Utambuzi/Ufahamu ambao tunao.
Tatizo la sayansi limekuwa kwamba kitu pekee ambacho mwanasayansi anaweza kukubaliana nacho ni kile alichodhibitisha au kukishika.

Falsafa imekuwa inatupa majibu ya maswali magumu kwenye maisha. Maswali kama tumefikaje hapa tulipo na tupo hapa duniani kufanya nini. Haya ni maswali ambayo sayansi imeshindwa kuyatolea majibu ya uhakika.

Maswali haya yanahitaji utambuzi wa hali ya juu, ambao upo ndani ya akili ya binadamu pekee. Hakuna kompyuta yoyote, licha ya kompyuta kuwa na uwezo mkubwa, ambayo inaweza kujibu maswali haya magumu ya maisha.

Wanasayansi wanasema tupo hapa duniani kujilinda na kuzaliana? Na wanafalsafa wanauliza, hilo linatutofautishaje sisi binadamu na minyoo?
Falsafa ndiyo inaweza kutupa majibu ya maswali haya magumu, ya kuhusu uwepo wetu hapa duniani.

Tuna ufahamu na utambuzi, ili kuweza kuishi maisha yenye maana kwetu na kwa wale wanaotuzunguka pia. Pia utambuzi huu tu apaswa kuutumia kuielewa dunia vizuri na hata kuwaelewa wengine, ili kuiwezesha dunia kuendelea kuwa sehemu salama.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa