KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 133 – 142.
Wanafalsafa wa kushuku (Skepticism) wanatuambia kwamba, changamoto kubwa tunazotengeneza kwenye maisha yetu ni kwa sababu tunajipa uhakika kwenye vitu ambavyp hatuna uhakika navyo.
Hata kama jambo tumeona linatokea kila mara na tumeshazoea haimaanishi ni uhakika.
Kwa mfano japo tumekuwa tunaona jua linachomoza mashariki kila siku, haitupi uhakika wa asilimia 100 kwamba kesho litachomoza mashariki.
Tukiweza kuondoka kwenye mtego huo wa kujipa uhakika kwenye vitu visivyokuwa vya uhakika, tutapunguza matatizo mengi.
Wanafalsafa wa kushuku wanatuambia tunapaswa kushuku kila kitu, kuhoji na kutafiti zaidi. Kwa sababu vitu vingi tunavyochukua kama ukweli siyo ukweli bali ni mazoea.
Shuku kila kitu, chunguza kila kitu na kuwa tayari kujifunza zaidi. Ukishaanza kujipa uhakika juu ya jambo lolote, unachagua kutokuujua ukweli.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa