KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 167 – 176.
Miaka mingi iloyopita, mwanafalsafa Plato alisema kwamba sisi binadamu tuna nafsi zaidi ya moja.
Na kinachofanya maisha yetu kuwa magumu, niale tunaposhindwa kudhibiti kila nafsi na kujikuta tunataka kuirishisha kila nafsi.
Miaka ya karibuni, sayansi hasa kwa upande wa saikolojia imegundua kwamba akili yetu imegawanyika katika sehemu tatu;
Sehemu ya kwanza ni ile inayofanya maamuzi ya kufanna kupona, maamuzi yale muhimu na inafanya kazi kama mjusi.
Sehemu ya pili ni ile inayohusiana na hisia na inafanya kazi kama wanyama.
Sehemu ya tatu ni ile inayofanya maamuzi makubwa na muhimu, hii ndiyo akili ya kibinadamu.
Sasa ili tuweze kutawala sehemu hizi za akili na kudhibiti maisha yetu, lazima tutumie akili zetu zenye uwezo wa kufikiri makubwa.
Lazima tuweze kuvuka kufanya maamuzi ya haraka na kuepuka kufanya maamuzi ya hisia.
Tunapaswa kufikiri kwa kina, na kuweza kuchukua hatua za kufanya mambo yawe vizuri zaidi.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa