KITABU; PHILOSOPHY FOR LIFE AND OTHER DANGEROUS SITUATIONS : ANCIENT PHILOSOPHY FOR MODERN PROBLEMS / JULES EVANS
UKURASA; 187 – 196…
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunapenda kukubalika ndani ya jamii tunayoishi.
Na ili kuweza kukubalika, huwa tunaishi maisha ya kuiga.
Mambo mengi ambayo tunafanya, ni kwa sababu tumeona wengine wanafanya.
Tafiti nyingi zimeonesha watoto huwa wanaiga yale wanayoona kwa watu wakifanya.
Na uigaji wenye nguvu zaidi ni wa watoto kwa wazazi wao, hasa watoto wa kiume kwa baba zao.
Mwanafalsafa Plutarch aliyeandika kitabu Parallel Lives alionesha jinsi wanafalsafa na watu mashuhuri wa zamani walivyokuwa na watu ambao wanawaiga.
Kwa maana hii, kwa kuwa ni vigumu kuishi bila ya kuiga, basi ni vyema tukachagua mashujaa ambao tutakazana kufikia zile hatua walizofikia.
Mashujaa hao wanaweza kuwa hai na kujifunza kwao moja kwa moja, au wakawa watu wa miaka iliyopita na tukajifunza kupitia vitabu na maandiko yao.
Hatua yoyote ambayo unataka kupiga kwenye maisha yako, angalia mtu aliyeweza kuipiga kisha mtumie kama shujaa wa maisha yako.
Na katika hilo, tuzingatie haya muhimu;
1. Tuwe mfano mzuri kwa watoto wetu, tujue wanatuangalia na kutuiga zaidi kwa matendo yetu kuliko kusikiliza maneno yetu.
2. Tuwasaidie watoto kuchagua mashujaa wao, kadiri wanafanya hivyo mapema, ndivyo wanavyoweza kupiga hatua kubwa mapema.
3. Angalia sana wale wanaokuzunguka, vitu unavyosoma na hata taarifa unazofuatilia, maana zinamchango kwenye mafanikio ya maisha yako.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa