KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa; 207 – 216…

Kupitia kitabu hicho, tumeona falsafa mbalimbali ambazo kila moja ilikuwa na msingi wa maisha mazuri.
Lakini falsafa zote hizi zina chimbuko lake kutoka kwa mwanafalsafa Socrates ambaye aliamini sisi binadamu tuna uwezo mkubwa wakufikiri, tunaweza kubadilika na kuweza kujidhibiti.

Kumekuwa na jitihada za watu kutafuta mfumo mmoja rahisi ambao kila mtu akiufuata basi atakuwa na maisha mazuri.
Lakini hakuna mfumo huo.
Badala yake kila mtu anapaswa kujifunzana kujaribu mifumo mbalimbali iliyopo, kisha kuona upi unamvutia zaidi na kuishi huo kwa kuboresha zaidi.

Hakuna mfumo au falsafa moja ambayo inaweza kumfaa kila mtu.
Bali kila mtu ana mfumo au falsafa itakayomfaa.
Ni jukumu la kila mmoja wetu kufanyia kazi hili ili kuwa na maisha mzuri.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa