KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
Ukurasa; 17 – 26.
Pamoja na ushawishi mkubwa ambao Socrates amekuwa nao kwenye falsafa zote duniani, Socrates hakuwahi kuandika kitabu chochote.
Hakuna kitabu chochote ambacho kimeandikwa na Socrates.
Socrates aliamini kwamba, njia bora ya kujifunza na kuishi falsafa ni kuhoji na kunadiliana.
Alisema iwapo utakihoji kitabu, hakitakupa jibu jipya, kitaendelea kukupa majibu yale yale ambayo yapo kwenye kitabu kile.
Yale tunayojifunza sasa kuhusu Socrates ni kutoka kwa wanafunzi wake na marafiki zake wa karibu.
Mmoja wao ni Plato ambaye ameandika kazi nyingi sana za Socrates.
Mtindo wa kufundisha wa Socrates ulikuwa wa kuhoji na kujadiliana.
Alitumia muda mwingi kuwahoji watu, kuwataka wafikiri kwa kina, waumize akili zao mpaka wapate majibu sahihi.
Socrates alitoa muda wake wote kwenye falsafa, aliamini na kufundisha sana kuhusu urafiki, upendo na mtu kujitambua.
Socrates alisema mtu ana mahitaji madogo sana ya kuwa na maisha mazuri, hakuwa mtu mwenye mali, na mara nyingi alionekana kutembea peku.
Akiwa na umri wa miaka 27, alitangazwa kuwa mtu mwenye hekima kuliko wote Athens, hakukubaliana na hilo, hivyo alichukua jukumu la kuzunguka mji mzima kusaka mtu mwenye hekima kuliko yeye lakini hakumpata.
Lakini hilo halikumfanya ajione anajua, badala yake aliendelea kukiri kwamba hajui na hivyo kuwa tayari kujifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa