KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 27 – 36.
Kupitia mtindo wake wa mijadala, Socrates anatufundisha ya kwamba, zoezi muhimu sana ambalo kila mtu anapaswa kufanya ni kujijua yeye mwenyewe kwanza.
Anasema watu wengi hukimbilia kuomba ushauri wakati hawajajijua wao wenyewe, hivyo ushauri wowote wanapewa wanauchukua bila ya kuhoji, na hivyo hauwasaidii.
Socrates anatuambia iwapo tutachukua muda na kujijua sisi wenyewe, kujua uimara wetu na madhaifu yetu, kujua uwezo mkubwa ulipo ndani yetu, kujua kipi hasa tunachopenda, tutaweza kufanya maamuzi bora kabisa kwenye maisha yetu.
Socrates anashangaa kabisa iweje mtu anapoenda kununua kitu kama mnyama anamchunguza kwa kina kabla hajafanya maamuzi ya kununua, lakini inapokuja kwenye kufanya maamuzi muhimu ya maisha, hawajichunguzi, badala yake wanakimbilia kuchukua ushauri wa wengine.
Kabla ya kufanya maamuzi muhimu ya maisha yetu, ni vyema tukajijua sisi wenyewe kwanza. Na hili siyo zoezi la kufanya mara moja, ni zoezi la kufanya kila wakati tunapohitaji kufanya maamuzi muhimu ya maisha yetu. Tupate muda wa kuchimba ndani yetu na tutapata hekima kubwa kuhusu sisi wenyewe.
Tuache uvivu wa kutaka ushauri rahisi katika kufanya maamuzi muhimu ya maisha yetu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa