KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 81 – 90.

Changamoto kubwa ambayo watu wanayo, na imekuwepo tangu enzi za Socrates ni watu kuamini sana maoni ya wengine.
Watu wakishaambiwa kitu, hasa na watu ambao wapo juu yao, basi huchukulia kama ndiyo ukweli na lazima iwe hivyo.
Hata pale mtu anapoomba ushauri, anachukulia ushauri anaopewa kama ndiyo ukweli na kuutumia ulivyo.

Socrates alipinga hili na alimtaka kila mtu afikiri kwa kutumia akili yake. Mtu asikubali kusikiliza na kuchukua kila anachoambiwa au kusikia kama ukweli usiotilowa shaka, basi anajinyima fursa ya kujua zaidi.

Ili kutumia akili zetu katika kufikiri sawasawa;
Tuhoji kila tunachosikia, kuona au kusoma. Haijalishi kimesemwa au kuandikwa na nani. Kila kitu kinapaswa kuhojiwa na kuchunguzwa kama ni kweli na kwa namna gani kina msaada.

Pale tunapoomba ushauri, haimaanishi ushauri tunaopewa lazima tuutumie kama tulivyoupokea. Badala yake tuhoji na kuchunguza zaidi iwapo ushauri upe unatufaa kwa hali yetu, mazingira yetu na changamoto tunazopitia.

Maamuzi yoyote muhimu unayofanya kwenye maisha yako, hakikisha umeyafikiri kwa kina na kuamua kipi unafanyia kazi. Usifanye maamuzi kwa sababu ya maoni ya wengine bila kushirikisha akili yako.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa