KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 101 -110.

Socrates anasifika kwa mfano wake wa watu waliozaliwa na kukulia pangoni. Huku wakiwa wamefungwa minyororo wasiweze kugeuga. Wanaangalia ukuta na nyuma yao unakuja mwanga ambao unaonesha vivuli vya vitu kwenye ukuta.
Anasema watu hawa watakuwa wanaona vivuli vile ndiyo uhalisia.
Ikitokea mmoja wao amefungua minyonyoro ile na kuufuata mwanga, akitoka nje ya pango na kuliona jua, kwanza litamshangaza, kwa sababu mi kitu hajazoea kuona. Lakini baada ya muda atazoea hali ile mpya.
Lakini iwapo atarudi kwenye pango na kuwaeleza wale ambao amewaacha, watampinga na kumwona amepotoka. Wataendelea kuamini vile vivuli wanavyoona ndiyo uhalisia.

Hivi ndivyo watu wengi wanavyoishi kwenye jamii.
Wengi wanafanya mambo kwa mazoea, wakiamini ndiyo ukweli wenyewe.
Na hata pale wanapoelezwa ukweli na wale waliouona, hukataa na kuendelea kufanya kwa mazoea.

Ili kujua ukweli, ili kuona kile halisi, tunahitaji kutoa changamoto kwa kila ambacho tumezoea.
Tuache kufanya mambo kwa mazoea na badala yake tuhoji mpaka kujua ukweli halisi wa kile tunachofanya, au kuamini.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa