KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 141 – 150.
Socrates alisifika kwa kuhoji kila jambo mpaka kujua ukweli wake.
Alimhoji kila mtu kwa kila jambo.
Hapakuwa na mtu au kitu ambacho Socrates hakuhoji au kuchimba zaidi.
Jambo hili lilipelekea wananchi wengi wa Athens kukerwa na Socrates na hiyo ilipelekea kushitakiwa kwa kuwapotosha vijana na kuleta miungu wapya.
Katika hukumu yake Socrates alikuwa na nafasi ya kujitetea na kuepuka kuadhibiwa. Lakini hakutumia nafasi hiyo kujitetea, badala yake aliendelea kusema ukweli. Aliendelea kuhoji na kusema anachosimamia yeye ni ukweli na ukweli siku zote unachoma uongo.
Alieleza namna ambavyo maneno mengi ya uongo yamekuwa yabasemwa juu yake, mpaka watu wameyapokea na kuwa kama ukweli.
Hata marafiki zake walimpa mbinu za kuweza kutoroka ilinkuepuka hukumu, lakini yeye hakukubali aliendelea kusimamia ukweli.
Kusimamia kwake ukweli kulipelekea yeye kuhukumiwa kuuawa kwa makosa hayonya upotoshaji, japo kwa uhalisia haukuwa upotoshaji bali kusimamia ukweli.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa