Because a thing seems difficult for you, do not think it impossible for anyone to accomplish. – Marcus Aurelius
Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NGUMU KWAKO SIYO NGUMU KWA WENGINE…
Tumekuwa tunafanya kosa moja kubwa sana,
Kwa kufikiri kwamba kitu kigumu kwetu basi ni kigumu kwa kila mtu.
Na kama kitu sis hatuwezi, basi hakuna anayeweza, au hakuna anayepaswa kuweza.
Kwa fikra za aina hii tunashindwa kujifunza na pia tunapoona wengine wanaweza tunajisikia vibaya.
Kuondokana na hali hii, ni vyema kukubali kwamba kitu ambacho ni kigumu kwako, kinaweza kuwa rahisi kwa wengine.
Kile ambacho umeshindwa kufanya, wapo ambao wamekifanya vizuri sana.
Hivyo jukumu lako ni kuwatafuta na kujifunza kupitia wao.
Kwa sababu kama wao wameweza, kuna kitu wanajua ambacho wewe hujuo, ukikijua na wewe utaweza pia.
Uwe na siku njema sana ya leo rafiki yangu, ya kujifunza kutoka kwa wote walioweza.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa