Sitaki kuwa hasi lakini ukweli lazima ukae wazi, ya kwamba kama unatumiwa na wengine, huwezi kufanikiwa. Unaweza tu kusahau kuhusu mafanikio kama umekabidhi maisha yako kwa wengine na kuwapa wao majukumu ya kufanya kile wanachotaka kufanya na muda wako, nguvu zako, utaalamu wako na hata uzoefu wako.

Hatua ya kwanza kabisa ya mafanikio ni kuanza kujitumia wewe mwenyewe, kuepuka kutumiwa na wengine na kuanza kujitumia mwenyewe.

Ubaya wa dunia ni kwamba, unakupa kile unachopigania, na usipopigana kabisa, dunia itahakikisha unakuwa silaha ya wengine kupambana ili kupata kile wanachotaka.

Hapa unaweza kujiuliza kwamba lazima kila mtu aachane na ajira kwa sababu ajira unatumika?

Taaluma

Siyo lazima uachane na ajira kwa sababu unatumika, badala yake kataa kutumika kwenye ajira. Fanya kazi kwa sababu unatoa mchango wako kwa wengine, na siyo kwa sababu unalipwa kufanya.

Fanya kazi kutengeneza jina lako na kutoa mchango wako, na siyo kufanya kwa kuwa mtu mwingine amekupangia kufanya. Na hata kama umepangiwa, angalia sababu ya wewe kufanya, zaidi ya ile uliyopewa na wengine.

Watu wanaofanikiwa zaidi, ni wale wanaojua sababu ya kufanya kile wanachofanya, wanaojitoa ili kutoa mchango mkubwa kwa wengine na wanaotumia kila kilichopo ndani yao kuhakikisha wanatoa thamani kubwa kwa wengine.

SOMA, UKURASA WA 906; Jipe Sababu Ya Kujithamini…

Anza sasa kujitumia, ili uweze kutengeneza mafanikio makubwa kwako.

Kikwazo kikubwa cha wengi kushindwa kujitumia ni kutokujijua au kutokujitambua. Ukipewa gari lakini ukawa hujui kuliendesha, huna namna itakubidi utembee kwa miguu na kuacha gari ambayo ingeweza kukusaidia sana.

Hivyo jijue vizuri, jua uko vizuri wapi na wapi una changamoto. Kisha weka juhudi kubwa kuhakikisha unatumia ule uwezo uliopo ndani yako kuweza kufanya makubwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog