If you wish to be a writer, write. – Epictetus
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNATAKA KUWA, FANYA.
Kila mtu kuna kitu anataka kuwa, lakini wengi huishia kusema.
Labda unataka kuwa mfanyabiashara,
Au unataka kuwa mwandishi,
Au unataka kuwa mshauri,
Au unataka kuwa mtu mwema.
Yota hayo na mengine mengi, hayatatokea kwakusema, bali kwa kufanya.
Hata useme na kutamani mara nyingi kiasi gani, kama hutafanya, huwezi kuwa.
Lazima ukae chini na ufanya,
Na unapofanya, watu wanaona, na wao ndiyo watakuwa wa kwanza kukuita kile unachofanya.
Chochote unachotaka kuwa, anza kukifanya,
Kifanye kidogo kidogo, kifanye kila siku.
Na unapaswa kujua kwamba kusema ni rahisi, kufanya ni ngumu.
Ndiyo maana kuna wasemaji wengi kuliko wafanyaji.
Wewe fanya.
Uwe na siku njema sana kwako leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa