No man was ever wise by chance. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KILA KITU KINATENGENEZWA…
Hakuna kitu chochote ambacho kinatokea kwa yeyote kama bahati.
Kila kitu kinatengenezwa, kila kitu kinafanyiwa kazi, kila kitu kinahitaji juhudi.
Unataka kuwa na hekima, unahitaji kuweka juhudi kwenye kujifunza na kufanyia kazi unayojifunza.
Unataka kuongeza kipato lazima uweke juhudi kwenye shughuli unayofanya.
Unataka kuwa na familia bora lazima uweke juhudi kwenye malezi na mahusiano.
Unataka kuwa mtu bora lazima uweke juhudi kwenye kila kinachohusika na wewe.

Usimwone yeyote aliyepiga hatua kwenye lolote ukasema ana bahati.
Jua ameweka juhudi kufika pale.
Na wewe pia utaweza kufika kama utaweka juhudi.

Kaweke juhudi leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa