Begin – to begin is half the work, let half still remain; again begin this, and thou wilt have finished. – Marcus Aurelius
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Ni siku nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUANZA NI NUSU YA KUMALIZA…
Huwezi kuamini ni kwa jinsi gani watu wengi wamejizuia kufanikiwa maeneo mbalimbali ya maisha yao kwa sababu tu hawakuwa tayari kuanza.
Unakuta mtu ana mawazo makubwa na mzuri sana, ambayo kama akiyafanyia kazi basi yataweza kumfikisha kweye mafanikio makubwa.
Lakini inapofika kweye kuanza, sababu hazikosekani.
Kunakuwa na kila sababu kwa nini mtu asianze ndani ya kipindi alichojiambia ataanza. Hivyo anaahirisha akiamini baadaye atakuwa bora zaidi, anaamini baadaye mambo yatakuwa mazuri.
Lakini hilo huwa halitokei, mtu hawi tayari na mambo hayawi mzuri. Na mbaya zaidi, mambo yanaendela kuwa magumu.
Hivyo basi, njia pekee kua kuchukua hatua ya kutufikisha kule tunakokwenda, ni kuanza.
Anza hata kwa hatua ndogo, na kitendo cha kuanza tu, ni nusu ya kumaliza.
Ukiwea kuvuka ule ukinzani wa kuanza, basi unaweza kupiga hatua zaidi kufika kule unakotaka kufika.
Wanasema siku zote mwanzo ni mgumu, na ukishaweza kuvuka ugumu huo wa mwanzo, hakuna cha kukuzuia kufanikiwa.
Ni kitu gani kimekuwa kigumu kwako kuanza?
Kianze leo, kianze kwa hatua ndogo, kianze mara moja na utaweza kupiga hatua kubwa sana leo ya kufaikiwa.
Ni kipi unakwenda kuanza leo?
Uwe na siku bora sana,
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz