Kwa jinsi unavyochukua hatua hata kama ni ndogo sana, lakini huku ukiwa na mawazo chanya, hivyo ndivyo utakuwa upo kwenye mchakato wa kuyaendea mafanikio yako.

Kuna wakati unaweza ukajiona kama vile huendi mbele au unajiona umesimama kabisa kwenye maisha yako, lakini unatakiwa ujiulize kuna hatua ambazo unachukua?

Kama zipo hatua unazochukua na kila wakati unajilisha mawazo chanya, basi ujue upo kwenye mchakato wa kuendelea kusonga mbele na kufukuzia mafanikio yako.

Hata kama ikitokea unapata matokeo ambayo hukutarajia au mambo yako hayafanikiwi kwa haraka, lakini kama unachukua hatua, wakati wako wa mafanikio unakuja.

Mafanikio siku zote ni hatua na wala si tukio la mara moja. Hiki ndicho kitu unachotakiwa ukijue ni muhimu kuchukua hatua hata kama ni ndogo.

9ab09-australia_cliffdiver

Kufikia mafanikio yoyote uelewe unatakiwa kuwa na mawazo chanya, kuchukua hatua na kujifunza kipi ambacho kinafanya kazi na kipi ambacho hakifanyi kazi.

Inapotokea kizuizi au kikwazo wakati unachukua hatua pia unatakiwa kuelewa hayo ni mapito ambayo unatakiwa kuyapitia lakini lilokubwa ni wewe kusonga mbele.

Kwa kile unachokifanya endela kuweka juhudi, endelea kukifanya kila siku bila kuchoka, kwani ukwa kufanya hivyo ndivyo unayasogelea mafanikio yako.

Hakuna nguvu unayowekeza kwa juhudi zote inapotea bure. Yapo matunda au ipo faida ya nguvu zako ambayo lazima utaivuna.

Hutakiwi kusahau hata kidogo endelea kuweka juhudi huku ukiwa na mawazo chanya ambayo yatakusaidia kuweza ufanikiwa.

Kuweka juhudi endelevu pasipo kuwa na mawazo chanya huku ni sawa na kujidanganya kwani hutaweza kufanikiwa kwa viwango.

Weka juhudi kila siku na kwa chochote ukifanyacho,itakusaidia sana kuweza kusonga mbele na kufanikiwa kwako hata kama unaona mambo magumu kwako.

Jiulize ni nini au ni kitu gani ambacho unaona kinakuziua kufanikiwa? Weka juhudi kwa chochote kile hata kama kinaonekana hakiwezekaniki.

Kumbuka siku zote kama nilivyosema juhudi haijawahi kumwangusha mtu hata siku moja. Siri ya mafanikio ipo kwenye kuchukua hatua chanya endelevu bila kujali mazingira yoyote yale kama kuna kushinda au kushindwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http://www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com