Habari za leo rafiki yangu?

Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye mwaka wa mafanikio 2017/2018. Huu ni mwaka wa kipekee ambao unaweza kwenda kufanya makubwa na kuweza kupata matokeo bora kabisa kwenye maisha yako. Ni mwaka wa tofauti na miaka mingine ambayo umekuwa unaweka malengo na mikakati, ambayo huchukui muda katika kuifanyia kazi, unaachana nayo mara moja.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha sana kwenye mwaka wa mafanikio, ambapo kwa pamoja tunakwenda kujifunza, kuhamasika na kushirikiana ili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yetu.

Msingi Mkuu

Kwa nini mwaka wa mafanikio?

Swali muhimu ambalo kama mtu ni mgeni anaweza kujiuliza ni kwa nini mwaka wa mafanikio? Na la msingi zaidi litakuwa mwaka wa mafanikio ni nini?

Majibu ni kwamba mwaka wa mafanikio ni kipindi ambacho unajipima kwa hatua unazochukua kwenye maisha yako katika kufikia ndoto zako kubwa za maisha. Kama ambavyo kuna mwaka wa biashara, mwaka wa serikali na hata mwaka wa kitaaluma, tunahitaji kuwa na mwaka wa mafanikio, ambao tunakwenda kuweka juhudi katika kufikia maono makubwa ya maisha yetu.

Mwaka wa mafanikio ni kipindi ambacho kwa pamoja tunajifunza na kufuatiliana kwa yale ambayo tunayafanyia kazi, kuboresha zaidi ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha yetu.

Kwa nini 2017/2018?

Mwaka wa mafanikio tunauita 2017/2018, kwa nini hatusubiri kuanza tarehe moja ya kila mwaka ili tuende sawa na watu wengine wanapojipanga kwenye mwaka wao? Hili ni swali ambalo mtu unaweza kujiuliza, na kuona labda hii ni njia ya kuyafanya maisha yawe magumu.

Kwanza kabisa tunauweka mwaka wetu wa mafanikio uanze kipindi tofauti na wale ambao wanaanza miaka yao ya kawaida. Hii ni kwa sababu wakati ambao kila mtu anashangilia mwaka mpya umekuwa ni wakati ambao siyo mzuri kuweka malengo na mipango. Unakuwa ni wakati ambao kila mtu anakuwa na hamasa kutoka nje kwa kuwa kila mtu anaweka malengo na mipango ya mwaka mpya.

Lakini unapofanya zoezi hili kwenye kipindi ambacho ni tofauti kabisa, kipindi ambacho kila mtu anafanya yake na hakuna anayehangaika na mambo ya malengo na mipango, unaweza kujipanga vizuri, ukiwa na hamasa kutoka ndani yako na ukaweka mipango ambayo ni muhimu kwako.

Lakini pia mwaka huu wa mafanikio tunaufanya ndani ya kikundi ambacho kina watu wenye mtazamo chanya na hamasa kubwa ya mafanikio. Watu ambao wapo tayari kujifunza na kushirikiana na wengine katika kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri sana.

Hivyo tunapoanza mwaka wetu tofauti na watu walivyozoea kuanza kipindi cha mwanzo wa mwaka, tunatangulia kuweka misingi ambayo tutaifanyia kazi, misingi ambayo tunaielewa kweli na siyo kwa hamasa ambayo inaisha ndani ya muda mfupi.

Mwaka wa mafanikio tunaupimaje na unaanza lini?

Mwaka wa mafanikio hatutaupima kwa tarehe wala miezi, badala yake tunaupima kwa wiki. Kwa sababu wiki ndiyo kipimo kizuri sana cha muda kuliko siku au mwezi. Siku inaweza kuwa ndogo sana na usipoisimamia vizuri ni rahisi kuipoteza. Mwezi pia ni kipimo kirefu ambacho ukijisahau unakuta umeupoteza mwezi wako.

Hivyo mwaka wetu wa mafanikio tunauhesabu kwa wiki, yaani siku saba ambazo zina masaa 168. Nitakupa mnyumbuliko mzuri sana wa kuweza kutumia muda huu vizuri.

Mwaka wa mafanikio unaanza wiki ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja kwa kila mwaka. Huu ni wakati mzuri ambapo kila mtu ametulia na anasubiri mwaka uishe, watu wengi wanaanza kutulia na kusubiri sikukuu na wengine wameshakata tamaa na kusema wanasubiri mwaka mpya uanze ndiyo waanze na kasi mpya. Hii ina maana ukianza kwenye kipindi cha aina hii, ukiwa na kasi kubwa, una nafasi kubwa ya kuweza kufanya makubwa.

Kwa mfano kama unapanga kufanya mazoezi, ukienda eneo la mazoezi tarehe za mwazo za mwaka, utakosa kabisa nafasi, kwa sababu kila mtu amepanga kufanya mazoezi kwa mwaka huo. Lakini nenda tarehe za mwisho wa mwaka, utakuta waliopo ni wachache sana.

Mwaka wetu wa mafanikio 2017/2018 utaanza wiki ya kwanza ya mwezi wa 11 mwaka huu 2017 ambayo inaanza jumatatu ya tarehe 06/11/2017. Tutahesabu wiki moja baada ya nyingine mpaka tunapozimaliza wiki 52 za mwaka wetu wa mafanikio.

Nini kinatokea mwisho wa mwaka wa mafanikio?

Mwisho wa mwaka wa mafanikio, tunakuwa na semina kubwa ya kukutana pamoja, ambapo tunashirikishana yale tuliyofanya kwa mwaka unaoisha wa mafanikio, pamoja na kuweka mikakati ya mwaka mpya wa mafanikio. Mwaka huu 2017 tumeshakuwa na semina hiyo na tunakwenda kuuanza mwaka, semina nyingine itakuwa mwisho wa mwaka wa mafanikio 2017/2018, wiki ya mwisho au ya pili kutoka mwisho ya mwezi wa kumi 2018.

Unahitaji nini ili kuweza kushiriki kwenye mwaka huu wa mafanikio na kunufaika nao?

Ili kushiriki vyema mwaka huu wa mafanikio na unufaike nao, unahitaji kuwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Hili ni kundi la kujifunza na kushirikiana ambapo tunakuwa karibu, bega kwa bega mpaka mwaka unaisha.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unapata nyenzo mbalimbali za kuhakikisha mwaka wako wa mafanikio unakwenda vizuri kabisa. unapata mafunzo muhimu kabisa ya biashara, mafanikio, fedha, uwekezaji na hata falsafa na imani. Yote haya yanakuwezesha wewe kukamilika kimafanikio na kuweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Kupitia KISIMA CHA MAARIFA utanufaika na yafuatayo;

  1. Kuwa kwenye kundi la wasap ambapo utajifunza kila siku, kwa kuianza siku na tafakari ambayo itakufanya uyaangalie maisha kwa mtazamo sahihi.
  2. Kujifunza kupitia madarasa ya kila jumapili, kwenye mada mbalimbali na kujadiliana kwa pamoja, pia kupata shuhuda kutoka kwa wanamafanikio wengine.
  3. Kusoma makala kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA, ambazo huwezi kuzipata sehemu nyingine yoyote, ni mpaka uwe mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.
  4. Kushiriki semina mbili zinazofanyika kwa njia ya mtandao wa wasap kwenye kila mwaka wa mafanikio.
  5. Kushiriki semina kubwa ya kila mwaka inayofanyika kwa kukutana moja kwa moja, semina ya kuhitimisha mwaka wetu wa mafanikio.

KISIMA CHA MAARIFA ndiyo sehemu pekee ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuwepo ili aweze kupiga hatua zaidi kwenye maisha yake.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA na karibu sana tuanze mwaka wetu wa mafanikio 2017/2018.

Kama tayari upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tuendelee kuwa pamoja, nitaendelea kukupa maelekezo zaidi kuhusu mwaka huu wa mafanikio 2017/2018.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kufanya hivyo mara moja, kama upo makini na maisha yako na unajua kule unakokwenda. Hupaswi kuendelea kujichelewesha tena. Chukua hatua sasa na jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupiga hatua kimafanikio.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapaswa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= ada hii itadumu kwa miezi 12 tangu unapolipa. Ina maana ukilipa tarehe 31/10/2017 itaisha tarehe 30/10/2018.

Namba za kufanya malipo ya ada ya KISIMA CHA MAARIFA ni MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA 0717 396 253. Majina kwenye namba hizo ni AMANI MAKIRITA na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na utapewa maelekezo zaidi.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, sehemu sahihi kwako kuweza kupiga hatua kwenye maisha yako.

MUHIMU; Jumapili hii kwenye darasa la jumapili la KISIMA CHA MAARIFA, nitafafanua kwa kina kuhusu mwaka wa mafanikio 2017/2018 na kujibu maswali na majibu. Pia nitaeleza kwa ufupi yale maeneo ambayo tunapaswa kwenda kuyafanyia kazi ili kuweza kuwa na maisha ya mafanikio makubwa katika kipindi hichi. Darasa hili litakuwa jumapili ya tarehe 05/11/2017 kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku. Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kuweka juhudi kwenye kila unachofanya na uweze kufanikiwa. Kama bado hujajiunga, jiunge sasa kwa maelekezo niliyotoa hapo juu ili tuwe pamoja.

Kuna vitendea kazi vya mwaka wa mafanikio 2017/2018 ambavyo nitavitoa kwa wanamafanikio wote, hivyo hakikisha unakuwa mmoja wa wanamafanikio ili kvipata.

Karibu sana kwenye mwaka wa mafanikio 2017/2018, karibu sana tushirikiane pamoja katika mafanikio.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani.

www.kisimachamaarifa.co.tz