KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 17 – 26
Tumekuwa tunajichukulia kawaida na kuona uwezo wetu ni mdogo, lakini kwa uhalisia, uwezo wa kila mmoja ni mkubwa sana.
Hapo ulipo, una uwezo wa kujifunza na hata ubunifu. Ni uwezo ambao hauna ukomo wowote ule, ila ule tunaojiwekea wenyewe. Kwa kifupi ni kwamba, tuna akili kuliko tunavyofikiri.
Imezoeleka kupima akili kwa IQ kwamba mwenye IQ kubwa ndiyo mwenye akili.
Lakini kipimo hicho kina mapungufu makubwa mawili;
1. Kipimo hichi kinaonesha kwamba akili ni za kuzaliwa, yaani akili alizo nazo mtu ni alizozaliwa nazo. Hivyo kama umezaliwa huna akili basi huna namna ya kubadili hilo.
Tafiti zinaonesha kwamba malezi na mazingira yanachangia sana kwenye akili. Na mtu anaweza kuongeza IQ yake kupitia kujifunza.
- Akili ni zaidi ya hesabu na kukariri. Kipimo cha IQ kinapima eneo moja la akili ambalo bi kukariri na kukokotoa. Lakini zipo aina nyingine za akili, kama muziki, mahusiano na kadhalika. Wapo watu ambao hawapo vizuri kwenye kukariri na kukokotoa, lakini wapo vizuri kwenye maeneo mengine.
Tuna uwezo mkubwa, na tunaweza kutumia na kuendeleza uwezo huo. Kama tu tutachukua hatua ya kujifunza na kutumia akili zetu.
Hilo ndiyo tunakwenda kujifunza kwenye kitabu hichi.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa