It is not death or pain that is to be dreaded, but the fear of pain or death. – Epictetus

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo mazuri sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HOFU INATESA ZAIDI…
Mambo mengi tunayoyaogopa na kuyakwepa kwenye maisha, huwa yanatokea mara moja tu.
Vitu kama kifo, maumivu, kushindwa na kadhalika.
Yanatokea mara moja na yakishatokea, huwa hayana mateso kama tunavyofikiri.

Kitu kikubwa sana ambacho kinatutesa ni hofu ya mambo hayo.
Na hii ni kwa sababu hofu tunaishi nayo kwa muda mrefu, kabla hata ya tukio kutokea.
Hofu inakaa na wewe muda mrefu, halafu ubaya zaidi kile unachohofia kinaweza kisitokee kwa wakati unaotegemea kitokee.
Hivyo hofu inatesa zaidi kuliko tukio lenyewe ambalo tunahofia.

Wakati wowote unapokuwa na hofu na kitu ambachonbado hakijatokea, jikumbushe kwamba hofu hiyo haina msingi, badala yake chukua hatua ambazo ni sahihi na tukio litakapotokea, utakuwa na maandalizi sahihi.
Hofu pekee haiwezi kukusaidia kwa lolote, kuchukua hatua ndiyo kunakusaidia.

Uwe na siku njema sana ya leo, nenda kaiishi siku hii ya leo, weka hofu pembeni.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa