KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 27 – 36.
Kabla ya karne ya 14, dunia ilikuwa imedumaa.
Hakuna maendeleo au mabadiliko makubwa yaliyokuwa yakitokea.
Mambo yalikuwa ni yale yale, vita vya ukabila na udini.
Watu hawakuwa na uhuru wa kufikiri watakavyo. Badala yake walitengenezewa nini cha kufikiri.
Utawala na dini, ambavyo vilikuwa kitu kimoja, viliwafanya watu kutokuwa na ruhusa kabisa ya kuhoji.
Karne ya 14, palitokea ugonjwa wa tauni ambao uliua watu wengi sana. Hapa ndipo watu walistuka na kugundua walichokuwa wakifikiri au kuishi mwanzo hakikuwa sahihi. Hapa ndipo watu walipoanza kutafuta majibu sahihi badala ya kukubali majibu rahisi wanayopewa.
Na hapo ndipo ulipotokea Uamsho wa kwanza, uamsho wa karne ya 15 ambao ulitengeneza mabadiliko makubwa sana hapa duniani.
Uamsho huu ndiyo uliowafanya watu kama kina Michelangelo, Leonardo da Vinci na Raphael kuweza kuja na ugunduzi wa mambo makubwa na ya tofauti.
Sasa hivi tunaishi kwenye zama ambazo zinahitaji Uamsho mwingine, lakini uamsho wa sasa siyo wa nchi au eneo zima. Bali ni uamsho wa mtu binafsi.
Tunatoka kwenye zama ambayo kila kitu kilikuwa ni uhakika na sasa tunaishi kwenye zama ambazo hakuna chochote ambacho mtu ana uhakika nacho.
Tunahitaji kuwa na Uamsho unaoanzia ndani ya mtu na kumwezesha kuwa bora zaidi.
Uamsho wa zama hizi unahitaji mambo matatu muhimu;
1. Ujuzi wa kompyuta, tunaishi zama za taatifa, ujuzi wa kompyuta utakusaidia sana.
2. Akili inayokua na kukomaa. Unahitaji mtu wa kujifunza kila siku.
3. Kuijua na kuielewa dunia vizuri. Kika kinachotokea eneo lolote duniani, kina athari kwa kila mtu. Ujuzi wa dunia, utakusaidi kuweza kutumia fursa na nafasi mbalimbali.
Tunahitaji kufanya Uamsho kuwa sehem ya maisha yetu ya kila siku. Tusidumae wala kufanya kwa mazoea.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani