KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 37 – 46.

Maisha ya Leonardo da Vinci yalikuwa maisha ya tofauti kabisa.
Kwanza alizaliwa nje ya ndoa kitu ambacho hakikuwa kinakubalika katika kipindi chake.
Hivyo ilibidi alelewe na babu yake na siyo baba yake.
Hii ilimnyima fursa ya kujifunza kupitia baba yake, kitu kilichokuwa kawaida enzi hizo.
Baadaye Leonardo alipata nafasi ya kujifunza kupitia mchoraji maarufu wa enzi hizo ambapo alijifunza na kupenda uchoraji.
Leonardo alitumia muda mwingi kujifunza kuhusu muundo wa binadamu na viumbe wengine, urukaji wa viumbe hai na dhana nyingine nyingi za kisayansi.
Leonardo aliendesha maisha yake kupitia kudhaminiwa na matajiri au viongozi mbalimbali.
Leonardo aliweza kufanya kazi nyingi katika kipindi chake, lakini nyingi hazikukamilika.
Baadhi ya picha hizo ni picha maarufu ya Mona Lisa, chakula cha mwisho cha Yesu na wanafunzi wake na nyingine nyingi.

Hapa tunaona ni jinsi gani uwezo wa mtu hauwezi kuzuiwa na watu au mazingira.
Na mtu anapochukua hatua ya kutaka kuwa bora zaidi, hakuna kinachoweza kumzuia.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa