While we are postponing, life speeds by. – Lucius Annaeus Seneca
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa mwaka mpya wa mafanikio 2017/2018. Tuna nafasi bora sana kwetu ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA YANAKUACHA NYUMA….
Kitu kimoja ambacho watu wengi wako vizuri sana ni KUAHIRISHA MAMBO.
Unakuta mtu amepanga kufanya kitu, lakini inapofika wakati wa kutekeleza, anaona kuna kitu hakijakaa sawa, hivyo anaahirisha.
Kitu ambacho watu wengi wanasahau ni kwamba, unapoahirisha mambo, MAISHA YANAKUPITA, YANAKUACHA NYUMA.
Hii ni kwa sababu maisha yanakwenda kasi mno, hivyo unapoahirisha chochote, muda haukusubiri, muda unaendelea kwenda mbele, na hapo ndipo maisha yanapokuacha nyuma.
Chochote unachopanga kufanya, kifanye kwa muda uliopanga. Hata kama hutakifanya kwa ukamilifu, wewe anza kukifanya. Utakuwa umepiga hatua ya kwanza muhimu sana. Na utaenda sambamba na maisha.
Muda ni mfupi, muda unakwenda kasi, fanya kile ulichopanga kufanya, kwa wakati uliopanga kufanya.
Nakutakia siku bora sana ya leo, nenda kafanye kila ulichopanga kufanya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa