If evil be spoken of you and it be true, correct yourself, if it be a lie, laugh at it. – Epictetus
Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera sana kwa siki hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UBAYA UNAPOONGELEWA JUU YAKO…
Kama upo hai, basi jua kitu kimoja, yapo mengi mabaya yatasemwa juu yako. Watu watakusema kwa ubaya, ambao unaweza kuwa kweli au usiwe kweli.
Tumekuwa tunafanya makosa makubwa kugombana na hata kuwachukia wale wanaotusema kwa ubaya. Tunawaona ni watu wabaya na wasiokuwa na mapenzi mema na sisi.
Leo nakwenda kukushirikisha njia bora kabisa ya kuchukua pale ubaya unapozungumzwa juu yako.
Kama ubaya uliosemwa ni kweli, basi jirekebishe. Chukua hatua kuhakikisha hufanyi tena kile ambacho siyo kizuri ambacho wengine wamekusema nacho.
Kama ubaya unaosemwa ni uongo cheka, cheka kwa sababu wanaosema ubaya huo ambao hauna ukweli ni wapumbavu. Hivyo hata kama utahangaika nao, haitasaidia lolote, utapoteza muda wako.
Je hii siyo rahisi zaidi?
Je huoni kwa njia hii utaepuka kabisa kugombana na watu?
Je huoni kwa njia hii utawafanya watu wakuheshimu na kuogopa kusema ubaya usio kweli juu yako?
Jirelebishe kama ni kweli, cheka kama ni uongo. Hii itakufanya kuwa bora, na kuuepusha na matatizo yasiyo na maana.
Ukawe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa