KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 124 – 133.

Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuelewa iwapo Leonardo da Vinci alikuwa mwanasayansi aliyejihusisha na sanaa au msanii aliyejihusisha na sayansi.
Hii ni kwa sababu alikuwa vizuri sana maeneo yote mawili. Alikuwa vizuri kwenye sanaa na kwenye sayansi pia.
Hivyo tunaweza kusema, Leonardo alikuwa msanii na mwanasayansi kwa wakati mmoja.

Kilichofanya michoro ya Leonardo kuwa na uhalisia na kupendwa na wengi ni ujuzi wake juu ya sayansi ya viumbe hai. Leonardo hakuchora tu kwa kufikiria, bali kwa kujua jinsi kitu kilivyo.

Sayansi na sanaa ni vitu viwili vinavyokwenda pamoja. Huwezi kuielezea sayansi kama huna sanaa. Na chimbuko la sanaa ni sayansi.

Kwa kuwa kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa ndani yake, basi tunapaswa kutumia uwezo huu kuweza kuwa vizuri kwenye maeneo yote makuu mawili ambayo ni sayansi na sanaa.

Hakikisha kwenye maisha yako ya kila siku, kwenye kazi na biashara zako, unatumia sayansi na sanaa ili kuweza kupata matokeo mazuri.
Sayansi inakuwezesha kufikiri kwa umakini na kina, kufikiri kwa kutumia mawazo zaidi.
Sanaa inakuwezesha kufikiri kwa ubunifu na kutengeneza kiti ambacho hakijawahi kuwepo kabisa.
Unapochanganya sayansi na sanaa, matokeo yake yatakuwa bora zaidi.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa