Neither should a ship rely on one small anchor, nor should life rest on a single hope. – Epictetus

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Tumepata nafasi nyingine nzuri leo ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIWEKE MATUMAINI YAKO SEHEMU MOJA….
Kinachofanya maisha yetu yaende, licha ya changamoto na kukosa uhakika, ni matumaini. Matumaini yanayupa nguvu ya kuchukua hatua ili kuwa bora zaidi.
Lakini watu wengi wamekuwa wanafanya kosa kubwa kwenye maisha yao, kwa kuweka matumaini yao kwenye eneo moja.
Hivyo inapotokea changamoto yoyote pale mtu alipoweka matumaini yake, inamharibia mtu huyo.

Weka matumaini yako kwenye maeneo mbalimbali na tofauti. Hasa inapokuja kwenye shughuli za kujiingizia kipato na hata watu unaowategemea kwenye shughuli zako.
Inapotokea eneo moja limekwama, maeneo mengine yanakuwa vizuri.

Kama ambavyo meli haitegemei nanga moja, nawe pia usiweke mategemeo ya maisha yako eneo moja.
Ukawe na siku bora sana leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa