KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 134 – 143.
Ubongo wa binadamu umegawanyika kwenye sehemu mbili, ubongo wa kulia na ubongo wa kushoto.
Ubongo wa kulia unahusika zaidi na mambo ya ubunifu na sanaa.
Ubongo wa kushoto unahusika zaidi na fikra na taratibu mbalimbali.
Watu pia wamegawanyika kwenye makundi mawili kulingana na ubongo upi ndiyo unatawala.
Wale ambao ubongo wa kushoto ndiyo unatawala, yaani una nguvu zaidi, huwa ni watu ambao wanapenda kufikiri sana, wanapenda kutengeneza na kufuata taratibu. Mambo yao yapo kwenye mpangilio maalumu na hupenda kuweka vitu kwa orodha.
Wale ambao ubongo wa kulia ndiyo unaotawala, yaani wenye nguvu zaidi, huwa ni wabunifu na wanapenda sanaa. Hawa hupenda kufanya vitu mbalimbali, hupenda kujaribu mambo mapya, hawana mpangilio maalumu wa mambo yao na kama wanaweka vitu, huchanganya na siyo kwa orodha.
Ni muhimu ukajijua unatumia zaidi ubongo upi ili uweze kutumia vizuri uimara ulionao.
Wengi huwa wanafikiri kama hawana mpangilio basi wana matatizo. Kumbe inawezekana wao wanatumia zaidi ubongo wa kulia.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa