KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 144 – 153.
Huwezi kutenganisha mwili na akili,
Mwili ukiwa na afya bora, akili inaweza kufikiri kwa kina.
Mwili ukiwa na afya mbovu, akili haiwezi kufikiri vizuri.
Moja ya mambo yaliyomwezesha Leornado kuwa vizuri kwenye fikra ni afya njema ya mwili.
Leornado alikuwa na mwili imara na wenye nguvu kubwa.
Hayo yote aliweza kutokana na kuzingatia mambo mawili muhimu.
Kuwa makini na chakula anachokula na kuwafanya mazoezi ya viungo.
Ni muhimu kula kwa kiasi na usishibe sana na kufanya mazoezi kwa kiasi na usijiumize.
Mwili wako ndiyo hekalu la akili yako, ambayo ndiyo inakuwezesha kufanya makubwa.
Linda mwili na akili yako ili kuweza kufikiri kwa kina na kufanya makubwa.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa