We are too much accustomed to attribute to a single cause that which is the product of several, and the majority of our controversies come from that. – Marcus Aurelius

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Ni siku nyingine nzuri, siku ya kipekee, siku bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SIYO KITU KIMOJA KINACHOSABABISHA…
Ni kawaida yetu binadamu kufikiri kwamba, jambo lolote linalotokea, basi limesababishwa na kitu kimoja.
Tunafikiri kwamba tukishajua kitu hicho kimoja basi tunamaliza kabisa kila tatizo tulilonalo.
Ni mpaka pale ambapo mtu anafanyia kazi kile pekee anachofikiri ndiyo kinasababisha anagundua kuna vitu vingi zaidi vinahusika.

Kila tatizo,
Kila mafanikio
Na kila hali,
Imesababishwa na vitu vingi, ambavyo kwa pamoja ndiyo vimezalisha kile kinachoonekana au kinachotokea.

Kunaweza kuwa na kitu kimoja kikubwa, ambacho kinachangia kwa nafasi kubwa, lakini hakiwezi kuwa chenyewe.
Hivyo unapotaka kutatua tatizo, unapotaka kupiga hatua au unapotaka kuondokana na kitu fulani, usikimbilie kutafuta sababu moja, bali tafuta sababu zote zinazohusiana na kitu hicho.

Uwe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa