Habari rafiki?

Miaka kadhaa iliyopita nilijipa jukumu moja kubwa la kuhakikisha kila anayekutana na mimi, iwe ana kwa ana au kupitia kazi zangu basi asibaki kama alivyokuwa awali.

Nashukuru wengi wamekuwa wakinipa mrejesho kwamba kazi zangu zimekuwa zinawasaidia kwa njia mbalimbali.

Msingi Mkuu

Wapo watu ambao wamekuwa wakipenda kunufaika zaidi kupitia huduma ninazotoa na hapa nimeorodhesha huduma zote za ukocha ninazotoa na utaratibu wake.

  1. AMKA MTANZANIA.

Hii ndiyo blog mama ya mafunzo yote ninayotoa. Hii ni blog yenye makala nyingi za biashara, kazi, mafanikio, mahusiano na hata uwekezaji. Kupitia blog hii, kila siku unapata makala nzuri za kukuwezesha wewe kuwa bora zaidi, kufanya maamuzi bora zaidi na kupiga hatua kwenye maisha yako.

Blog hii ni bure kabisa kuisoma na itaendelea kuwa bure daima. Tembelea www.amkamtanzania.com kila siku kujifunza.

Pia unaweza kujiunga na mfumo wa kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako, ambao ni bure pia. Fungua; www.subscribepage.com/jiungeamka  kujiunga na mfumo huu wa kupokea makala kwa email.

Lipo kundi la Telegram la AMKA MTANZANIA, ambapo ndani yake unajifunza mambo mbalimbali kupitia waandishi na walimu mbalimbali. Kujiunga na kundi hili, bonyeza; https://t.me/joinchat/AtuDbT5VoqpCYiIPEexFDw

  1. KISIMA CHA MAARIFA.

Huduma nyingine ya mafunzo na ukocha ninayotoa ni kupitia KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye KISIMA kuna blog ambayo ina makala nyingi na nzuri za mafanikio, kazi, biashara, uwekezaji, falsafa na uchambuzi wa vitabu. Pia lipo kundi maalumu la wasap ambapo kila siku kuna mambo mazuri ya kujifunza.

Kupitia kundi la wasap, kila siku asubuhi unaianza siku yako kwa TAFAKARI, kila jioni tunashirikishana yale tuliyojifunza na kila jumapili tunakuwa na madarasa ya jumapili ambapo tunajifunza kwa kina mambo mbalimbali kuhusu mafanikio kwa ujumla.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapaswa kulipa ada ya tsh 50,000/= kwa mwaka. Ada hii inaisha miezi kumi na mbili baada ya mwezi uliolipia.

Unaweza kutembelea blog ya KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza www.kisimachamaarifa.co.tz Utaziona makala lakini hutaweza kuzifungua mpaka uwe umejiunga na kuwa mwanachama.

Kujiunga tuma fedha tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 (Majina yanayotokea ni AMANI MAKIRITA). Ukishatuma ada tuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako na kwamba unajiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwenye namba 0717 396 253.

  1. PERSONAL COACHING.

Hii ni huduma ambapo mimi nakuwa kocha wako moja kwa moja kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kupitia huduma hii, unakuwa na kitu ambacho unapanga kukifanyia kazi lakini umekuwa unaahirisha au huna hamasa ya kuanza na kuendelea.

Kupitia personal coaching tunafanya kazi kwa karibu na ninakufuatilia kuhakikisha unafanya kile ambacho umepanga kufanya.

Gharama ya huduma hii ni tsh 100,000/= kwa mwezi. Ada hii unailipa kabla ya coaching kuanza na inalipwa mara moja yote.

Iwapo kuna kitu unataka kufanya, tabia unataka kubadili au mambo unataka kuyabadili, lakini unashindwa kuanza au ukianza unaishia njiani, personal coaching itakusaidia sana.

  1. GAME CHANGERS.

Hii ni huduma ya ukocha ambayo naitoa kwa kikundi cha watu watano kwa pamoja. Kupitia huduma hii, watu watano ambao kila mtu ana kitu anataka kufanyia kazi au hatua anataka kupiga, nawaweka kwenye kundi moja na wanakuwa wanafuatiliana kwa karibu kila mmoja.

Kundi hili naliendesha kwa mfumo wa MASTERMIND GROUP ambapo unapata ile faida ya wengine kukuhoji kwa kina na kukufuatilia kwa kile ambacho unakifanya. Mimi nakuwepo ndani ya kundi kutoa msaada na mwongozo wa namna watu wanapaswa kwenda.

Pia mara moja kila wiki tunakuwa na simu ya pamoja (conference call) ambapo tunakuwa kwenye simu ya pamoja wote, kila mtu anaeleza yale anayofanyia kazi, anahojiwa kwa kina na wengine na kutoa mrejesho wa yale anayofanyia kazi, au aliyoshauriwa kufanyia kazi kipindi kilichopita.

Huduma hii ya ukocha ya GAME CHANGERS inatolewa kwa misimu, hivyo nakuwa natangaza kipindi cha watu kujiunga na huduma hii.

Huduma hii ni kwa wiki 5, ambazo watu wanafanya kazi pamoja na kuhakikisha ndani ya wiki hizo tano kila mtu anaondoka na kitu alichofanya au kuzalisha.

Gharama ya huduma hii ni tsh 200,000/= ambayo ni kwa kipindi hicho cha wiki 5. Ada inalipwa kabla ya huduma kuanza na inalipwa yote kwa pamoja.

  1. LEVEL UP.

Hii ni huduma maalumu ya ukocha kwa wale watu ambao wanataka kupiga hatua kubwa kabisa kwenye maisha yao. Hii ni maalumu kwa wale watu ambao wamefanikiwa halafu mafanikio yakawa mtego kwao. Yaani mtu anakuwa amepiga hatua kwenye maisha yake, lakini akafika sehemu ambao anaona hapigi hatua tena. Anakuwa amedumaa na hana tena hamasa ya kusonga mbele.

Huduma hii naitoa kwa mtu mmoja mmoja ambaye nafanya naye kazi kubwa na kwa karibu sana kwa kipindi cha wiki 10. Katika wiki hizi kumi, tunatengeneza kabisa upya mfumo wa mtu wa kufikiri, tunatengeneza mpango mpya wa kufanyia kazi na kuufanyia kazi kuhakikisha hamasa inarudi upya na mtu anaendelea kuweka juhudi.

Gharama za huduma hii ya LEVEL UP ni tsh 1,000,000/= kwa kipindi chote cha wiki 10. Ada hii unalipa tsh 100,000/= kila wiki, kabla ya wiki husika kuanza.

Hizi ndizo huduma muhimu ninazotoa kwako rafiki yangu, kuhakikisha kwamba natimiza kusudi langu la kuhakikisha kila mtu anakuwa bora zaidi.

Ada hizi nilizoweka ni kiasi kidogo kulingana na muda na juhudi ambazo ninaweka hasa pale ninapofanya kazi na mtu mmoja mmoja.

Pia hutapoteza fedha yako, unapolipia huduma yoyote, halafu ukaanza kutumia huduma hiyo na ukaona haikufai au haikuwezeshi kupiga hatua, basi unaniambia na ninakurudishia fedha yote uliyolipa, bila kukukata hata shilingi moja. Hizi ni huduma nitakazoendelea kuzitoa kwa muda mrefu hivyo ninachokazana ni kutoa thamani kubwa kwa kila mtu, ili kila anayepata huduma ninayotoa, awe balozi mzuri.

Ninachopenda kuwashauri watu wengi ni kabla hujalipia huduma za juu ambazo gharama yake ni kubwa, anza na huduma za chini. Kwa mfano kama huna fedha kabisa ya kulipia huduma anza na huduma ya bure ya AMKA MTANZANIA. Ukishaanza kupata matokeo mazuri ndiyo unaendelea kulipia huduma nyingine zinazoendelea. Kabla hujalipia huduma ya PERSONAL COACHING AU GAME CHANGERS, lipia kwanga kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa njia hii utakuwa kwenye mazingira sahihi ya kunufaika na yale unayolipia na unayojifunza.

Mwisho, kitakachokupa nafasi ya kuingia kwenye huduma hizi siyo fedha ulizonazo, bali utayari wako kujifunza na kupiga hatua. Usishangae ukaomba baadhi ya huduma hizo na nikakuambia huwezi hata kama una fedha za kulipia. Lengo lango siyo tu kupata fedha zako, bali kuhakikisha kitu unachopata kinakusaidia. Kama bado hujawa tayari, nitakuambia na yapi ufanyie kazi.

Kwa mawasiliano ya jinsi ya kupata huduma yoyote kati ya hizi, tuwasiliane kwa simu; 0717 396 253 au 0755 953 887. Pia unaweza kuniandikia email kwenye amakirita@gmail.com

Karibu sana rafiki yangu, tufanye kazi pamoja ili kila mmoja wetu aweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yake. Nina mengi ya kukushirikisha, lakini pia ninazo mbinu za kukuwezesha wewe upige hatua zaidi. Kwa ngazi mbalimbali za huduma ninazotoa, utaweza kunufaika na mambo hayo.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Daktari wa binadamu, kocha wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali.

www.amkamtanzania.com / www.kisimachamaarifa.co.tz

MIMI NI MSHINDI