A kingdom founded on injustice never lasts. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari BILA MISINGI YA USAWA, KILA KITU KINAANGUKA….
Unaweza kujenga chochote kwa haraka bila ya kuzingatia misingi ya usawa.
Lakini matokeo yake huwa ni kuanguka kwa kitu hicho.
Hilo huanzia kwenye maisha ya mtu binafsi mpaka ngazi ya dunia nzima.
Kama mtu atajenga maisha yake kwa misingi isiyo ya usawa, yataanguka.
Kama mtu atajenga mahusiano yake na wengine kwa misingi isiyo ya usawa, mahusiano hayo yatavunjika.
Kama mtu atajenga biashara yake kwa misingi isiyo ya usawa, itashindwa.
Na kama taifa litajengwa kwenye misingi isiyo ya usawa, litaanguka.

Dunia inajiendesha kwa misingi ya usawa, misingi ambayo huwezi kuivunja na ukabaki salama.
Dunia inataka KUTOA NA KUPOKEA, na siyo kupokea tu au kutoa tu.
Chochote kinachojengwa kwenye misingi isiyo ya kitoa na kupokea, kinavunjika, hakidumu kamwe.

Chochote unachofanya kweye maisha yako, fanya kwa misingi ya usawa, na kitadumu kwa muda mrefu.
Ukawe na siku bora sana leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
http://www.amkamtanzania.com/kurasa