KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 164 – 173.

Licha ya kuwa msanii na mwanasayansi, Leonardo da Vinci pia alikuwa mshauri wa mambo mbalimbali ikiwepo imani, mahusiano na hata maadili.
Ufuatao ni ushauri wa Leonardo kuhusu kuwa na maisha bora.

KUHUSU MALI NA TAMAA.
💥Usijiahidi au kufanya kitu ambacho kama utakikosa basi utateseka kwa kukikosa.
💥Furaha ni hali ambayo inaanzia ndani ya mtu mwenyewe.
💥Kwa wenye tamaa, hawaridhishwi na chochote na hivyo kushindwa kufurahia uzuri wa dunia.
💥Yule mwenye umiliki wa mali nyingi, ndiyo mwenye hofu ya kupoteza zaidi.

KUHUSU MAADILI NA MAJUKUMU BINAFSI.
💥Usawa unahitaji nguvu, utashi na utambuzi.
💥Asiyeadhibu kosa, analitetea.
💥Hakuna uliye na mamlaka naye, wala aliye na mamlaka na wewe ila wewe mwenyewe.
💥 Anayetembea kwa unyoofu ni mara chache sana anaanguka.
💥Mtu anapaswa kusifiwa au kulaumiwa kwa yale yaliyopo ndaninya uwezo wake.

KUHUSU MAHUSIANO.
💥Omba ushauri kwa yule anayeweza kujisimamia vizuri.
💥Kumbukumbu ya faida ni fupi kuliko ya kukosa shukrani.
💥Mkosoe rafiki faraghani, msifie hadharani.
💥Uvumilivu unazuia matusi kama nguo inavyozuia baridi.

KUHUSU UPENDO.
💥Kufurahia kipende kitu kama kilivyo na siyo kwa sababu yoyote ile.
💥Mapenzi yetu kwenye kitu ndiyo chanzo cha maarifa juu ya kitu hicho.
💥UPENDO UNASHINDA KILA KITU.

Tuyazingatie maadili haya ya Leonardo na kuyaishi kwenye maisha yetu ya kila siku.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa