Everything that happens happens as it should, and if you observe carefully, you will find this to be so. – Marcus Aurelius
Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Ni siku nyingine mpya ma ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KILA KINACHOTOKEA NI KAMA KINAVYOPASWA KUTOKEA…
Kila mtu huwa anakuwa na matarajio fulani,
Kila mtu anafanya mambo kwa mategemeo fulani.
Lakini mara nyingi, matokeo tunayopata huwa ni tofauti kabisa na yale tunayotegemea.
Kwa hali kama hii tunaweza kufikiri tuna bahati mbaya au hatuna bahati.
Lakini ukweli ni kwamba, kila kinachotokea, kinatokea kama kinavyopaswa kutokea.
Kama umeweka juhudi zote, kama umefanya kila unachopaswa kufanya, na matokeo yakaja tofauti, usiumie.
Jua kwamba yale matokeo uliyopata, ndiyo imekupasa kupata kulingana na juhudi ulizoweka na mazingira yanayokuzunguka pia.
Hivyo kupata matokeo tofauti, unahitaji kuweka juhudi tofauti na kuwa kwenye mazingira tofauti.
Jifunze kwa kila unachopitia, hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha